HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 9, 2018

MHANDISI ULANGA ACHUKULIWA HATUA

 Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka mara baada ya kukagua tenki la mradi wa maji wa Gombe, wilayani Ulanga, mkoaniMorogoro.
   NaibuWaziriwaMajinaUmwagiliaji, JumaaAweso (kushoto)naMbungewaJimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga wa kiwa kwenye moja ya kichoteo cha maji cha mradi wa maji wa Gombe ambacho hakitoimaji.


  Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa  Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji akiipeleka kwenye nyumba iliyopo katika Kijiji cha mara baada ya kuzindua mradi huo wavisima 27.
Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Jumuiya yaWatumiaji Maji katika Kata yaLupiro, Wilaya ya Mahenge, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amechukua hatua za kinidhamu kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Interconsult kutokana na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Gombe uliopo Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri ameagiza vyombo vya usalama kumkamata na kufanya uchunguzi kwenye mradi huo wa Gombe ambao umechelewa kukamilika licha ya asilimia kubwa ya fedha kuwa zimeshalipwa kwa mkandarasi, lakini pia unakosa thamani halisi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wake.

Aweso alitoa maagizo hayo wakati alipokuwa ziarani katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro mara baada ya kupata taarifa ya kusuasua kwa mradi huo na wananchi wa Gombe kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.

‘‘Katika taarifa nimeambiwa kuwa mradi unatoa maji, lakini nimekuja kuona na si kweli wakati wizara imetoa fedha. 

Kama Naibu Waziri wa Maji sitakubali kusikia fedha za miradi ya maji zinaliwa kila ninapoenda, naagiza Mhandisi Mshauri akamatwe na uchunguzi ufanyike na endapo itabainika amehujumu achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wahandisi wote nchini’’, alisema Aweso. 

Amesema kuwa wizara itaandaa orodha ya majina ya wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na kuikabidhi kwa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi ili wafutiwe kabisa usajili na kutopewa kazi yoyote tena nchini endapo watathibitika kufanya hivyo.

Akiwa Ulanga Naibu Waziri Aweso amezindua ofisi ya maji ya Kata ya Lupiro, mradi wa maji wa visima 27 katika Kijiji cha Chikuti, ambacho ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo na kukagua skimu ya umwagilaji ya Mnepa, iliyopo Kata ya Lupiro. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad