HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 March 2018

KUWAIT YAZINDUA KISIMA CHA 61 KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI

Wanafunzi wakibeba galoni za maji zilizotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait nchini

Balozi wa Kuwait nchini  Jasem Al-Najema amezindua kisima cha 61 katika Shule ya Msingi ya GEZAULOLE Wilayani Kigamboni, Dar es salaam ikiwa ni mwendelezo wa utekelezezaji wa mradi wa '' KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE'' ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait mwishoni mwa mwaka 2016.

 Hafla ya uzinduzi wa kisima hicho ilihudhuriwa pia na Diwani wa Sumangila Francis M. Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maziku Luhemega, Mwenyekiti wa CCM Gezaulole Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shaaban pamoja wa walimu na wanafunzi wa Shule hiyo.

Kisima hicho kilichozinduliwa na balozi wa Kuwait Al-Najem kitanufaisha Shule ya Msingi ya GEZAULOLE iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na Shule jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushdy yenye wanafunzi 250 ilianzishwa mwaka 2007.

Balozi Al-Najem katika hotuba yake baada ya uzinduzi wa kisima amesema kuwa Ubalozi wa nchi yake umeanzisha mradi wa ''KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE'' ili kuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa Tanzania Mhe. John Magufuli  ya kutoa elimu bure. 
Balozi Al-Najem ahutubia hadhira baada ya uzinduzi wa kisima kulia kwake ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni mwalimu mkuu Maryam Shaban.

Al-Najem ameeleza kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo katika kutatua changamoto zinazokabili shule hiyo.

Aidha aliahidi kuwapatia wanafunzi wa Shule hiyo madaftari, mikoba na geloni za kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao kujihimu katika masomo yao ili wawe madaktari, wahandishi, walimu na watu wa fani mbalimbali baada ya kumaliza masomo yao hapo baadae.

Kwa upande wake Diwani wa Sumangila Francis M. Chichi ameishukuru Kuwait kwa kuchimba kisima cha maji katika Shule hiyo huku akimuomba Balozi Al-Najem kuisaidia Kata yake gari ya kubebea wagonjwa ili kuwaokoa akina mama wajawazito  na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika hospitilini na katika vituo vya afya ambapo baadhi ya wakati hulazimika kukodi pikipiki ili kufika huko jambo ambalo linahatarisha uhai wao.
Balozi Al-Najem akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (aliyevaa nguo nyekundu) na Sheikh Kaporo msimamizi wa ujenzi wa kisima (alievaa kanzu na kofia) azindua rasmi kisima cha maji katika Shule ya Gezaulole
Balozi akikagua moja ya madarasa ya shule ya Gezaulole akifuatana na viongozi wa serikali ya Mtaa na walimu ambao wamemfafanua hali halisi ya Shule na changamoto zinazoikabili
Balozi Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapatia madaftari na mikoba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad