HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 March 2018

MCHENGERWA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA JIMBONI KWAKE RUFIJI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Rufiji mkoani Pwani, Mohamed Mchengerwa amesema tangu amechaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo amefanikiwa kusukuma upatikanaji wa maendeleo na kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia utekelezaji wa ahadi za maendeleo ya wananchi na hasa katika elimu, miundombinu ya barabara, nishati ya umeme pamoja na maji safi na salama.

"Katika kipindi cha  miaka miwili ya ubunge kuna maendeleo mengi yamepatikana na haijawi kutokea.Hiyo yote inatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mimi mwenyewe katika kuelezea matatizo ya wananchi kwa Serikali,"amesema.

Amesema katika mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge utasukuma maendeleo ya wananchi wa Rufiji na kuongeza ajira kwa  wananchi katika kuinua uchumi wa jimbo hilo.Ujenzi wa mradi huo ulikuwa ni kilio cha muda mrefu lakini kutokana na Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa vitendo. 

Mchengerwa amesema ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge utakwenda pamoja na ujenzi wa daraja la Utete ambalo lilikuwa changamoto ya muda mrefu na kufanya baadhi ya huduma kwa jamii zishindwe kuendelea.

Amesema katika jitihada hizo Serikali imekarabati shule za msingi na sekondari pamoja hospitali, zahanati  na vituo vya afya.

Amesema katika kujenga afya za wananchi wa Jimbo la Rufiji ameandaa mashindano ya Mchengerwa Cup ambalo ltaanza siku za karibuni kwa kushindanisha timu mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Rufiji,  Rajab Mbonde amesema mbunge afanya kazi nzuri na kufanya viongozi wa Chama kutembea kifua mbele katika ukarabati wa ofisi yao ngazi ya Wilaya.
 Mwenyekiti wa Wilaya ya  Rufiji , Rajab Mbonde akizungumza na waandishi kuhusu utekelezaji wa ahadi za mbunge kama wasimamizi wa ilani ya Uchaguzi .
.Mbunge wa Rufiji , Mohamed Mchengerwa  akizungumza na waandishi habari kuhusu utekelezaji wa ahadi mbalimbali katika jimbo la Rufiji.

 Mbunge wa Rufiji , Mohamedi Mchengerwa akimkabidhi Katibu wa Chama cha Mpira wilayani Rufiji Yahya Kisangi kwa ajili ya Ligi ya Wilaya ya Mchengerwa Cup.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad