HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 12 March 2018

KESI YA WEMA UPANDE WA MASHTAKA WAFUNGA USHAIDI

Miss Tanzania 2006 na Msaanii wa filamu, Wema Sepetu akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri ya Madawa ya kulevya.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
BAADA ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa mlimbwende wa Tanzania 2006 na msaniiwa filamu hapa nchini, Wema Sepetu na wenzake watatu kunguruma kwa takribani mwaka mmoja, leo Machi 12, upande wa mashtaka umefunga ushahidi wao.

Hatua hiyo imekuja baada ya mashahidi watano wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wao na kuiachia mahakama katika maamuzi.

Baada ya mahakama kupata taarifa hiyo kutoka kwa Wakili wa serikali, Constantine Kakula, wakili wa Utetezi, Albert Msando aliiomba mahakama kuwasilisha hoja zao za kuishawishi mahakama kuwa washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu.

" Mheshimiwa tunaomba kujenga hoja kwa washtakiwa wote watatu kuwa hawana kesi ya kujibu kuhusiana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa na upande wa mashtaka, amedai Wakili Msando.

Kifuatia ombi hilo, Hakimu Simba ameutaka upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao Machi 23, mwaka huu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.

Kabla ya upande wa mashtaka kuifunga kesi yao waliwaita mashahidi wawili kutoa ushahidi ambao ni,  Steven Ndondo mjumbe wa shina namba 39 eneo la Basihaya na askari D 603 Ditektivu Koplo Robert (31).

Katika ushahidi wake,  Ndondo akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula amedai kuwa Februari 4,2017 saa 10 jioni alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu kuwa anahitajika mtaa wa Nazareti nyumbani kwa Wema kwa ajili ya kufanya upekuzi.

Amedai kuwa upekuzi ulianzia jikoni ambapo katika kabati la vyombo ulipatikana msokoto wa sigara ambayo hakuwa akijua ndani yake kulikuwa na nini, pia walikuta karatasi inayosadikiwa kuwa inatengenezewa mihadarati Mimi sihifahamu polisi ndiyo walisema Rizla.

Pia katika chumba cha kihifadhia nguo na viatu vya Wema walikuta kipisi cha sigara ambacho hakijulikani ni cha sigala ya aina gani.

Katika chumba cha wafanyakazi wa Wema kwenye kabati walikuta ganda la kiberiti ndani yake kukaonekana kipisi cha sigara.

Hata hivyo katika chumba cha kulala cha Wema katika upekuzi huo hawakuona kitu chochote.

Kwa upande wa Koplo Robert alidai kuwa Februari 4,2018 akiwa ofisini kwake polisi kati muda wa jioni alipewa Vielelezo msokoto mmoja, vipisi viwili vya msokoto ambayo vilikuwa ndani ya kiberiti vya majani yanayodhaniwa kuwa ni bangi.

Baada ya kukabidhiwa na Inspekta Wille alivihifadhi na kwamba alipewa kwa ajili ya kuvipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo Februari 6,2018 alivipeleka na kusajiliwa.

Ameeleza kuwa baada ya vipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali vilifanyiwa kazi na kureshwa polisi kuhifadhiwa na hadi sasa vipo polisi.

Mbali na Wema, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4, mwaka huu, katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad