HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 23 March 2018

DAMU SALAMA NA MEWATA WAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO

Chama cha madaktari wanawake Tanzania (MEWATA) kinaendesha kampeni (tarehe 22- 24 machi ) ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.  Kampeni hiyo ilizinduliwa na mke wa rais mstaafu Mhe. Mama Salma Kikwete Mbunge wa viti maalum, baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo, akinamama na wasichana mkoani Lindi, walipata fursa ya kufanya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya matiti na mlango
wa kizazi.
Mpango wa Taifa wa Damu Salama kanda ya kusini Mtwara unashiriki katika kampeni hiyo kwa kuendesha zoezi la kuchangia damu kwa wananchi wenye afya na vigezo vya kuchangia damu mkoani Lindi.
Akizungumza baada ya kuchangia damu Raisi mstaafu wa MEWATA Dkt. Marina Njelekela aliwaasa wananchi wenye uwezo na vigezo vya kuchangia damu wajitokeze kuchangia damu kwani mahitaji ni makubwa kutokana na ajali za barabarani na kina mama wakati wa kujifungua, Dkt. Marina aliendelea kusema “viwango wa kimataifa vinaelekeza mwanaume achangie damu kila baada ya miezi mitatu na mwanamke kila baada ya miezi minne”.

Kwa upande wa Damu Salama  Afisa mawasiliano na uhusiano wa Mpango bwana Rajab Mwenda alitoa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari na pia alikumbusha Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kushirikiana na Timu za damu salama halmashauri zinatarajia kuendesha kampeni ya mwisho ya robo mwaka (Januari- machi) tarehe 26- 30 machi nchi nzima hivyo aliomba wananchi waunge mkono kwa kujitokeza kuchangia damu.
 Dkt. Marina Njelekela akichangia damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.
Mhe. Mama Salma Kikwete akicheza nyimbo ya nani kama Mama ya Christian Bella baada ya uzinduzi wa Kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi iliyofanyika mkoani Lindi  katika hospitali ya mkoa ya sokoine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad