HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 12 March 2018

BENKI YA CRDB TAWI LA MLIMANI CITY WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA ZAWADI KWENYE WODI LA WALIOJIFUNGUA KWA UPASUAJI NA

 Baadhi ya Zawadi za benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya washindi wa Akaunti ya Malkia.WAFANYAKAZI wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam waadhimisha siku ya wanawake kwa kutoa zawadi katika wodi la wanawake waliojifungua kwa upasuaji pamoja na wenye kifafa cha mimba katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Saalaam.

Akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Malimani City, Adelpghina Barongo amasema kuwa wanawake wananchango mkubwa sana ndio maana wameona umhimu wa kutoa zawadi kwenye wodi hiyo kwana wanawake pia ndio wanaopata changamoto mbalimbali.

"Wanawake wanamchango mkubwa pia ndio wanaopata chamgamoto mbalimbali ndio maana tumeota tuwae zawadi japo kidogo wa akinamama ambao wapo hospitali"

Ametoa wito kwa akinamama waliopo hospitali kufungua akaunti kwaajili ya kujiwekea akiba kwani akaunti ya Malkia ni sawa na kibubu chenye dhamana pamoja na faida.

"Wanawake tujifunze kuweka akiba benki kuweka ndani hii haina ulizi wa pesa kutokana na majamga mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza kama moto na wizi  akauti hii inaulizi tosha na madhibuti"Amesema Adelphina.

Benki ya CRDB yenye kauli mbiu ya siku ya Mwanamke Tanzania isemayo "Mwanamk na Malkia akaunti"  pia kauli mbiu ya Kitaifa ni Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”. hii inawaa nguvu benki hiyo kuendelea kuwaangalia wanawake kwa jicho la karibu zaidi kwani wanajua mchango wa mwanamke kwa jamii.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlima city wakiwa katika hospitali ya Mwananyamala wakiwa tayari kutoa msaada katikawodi ya wanawake waliojifungua kwa upasuaji na wenye kifafa cha mimba katika hospitali  hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuwajali wanawake na watoto kuadhimisha siku ya wananwake duniani ambayo hufanyika Machi nane kila mwaka.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja leo.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Mwananyamala wodi ya wanawake waliojifungua kwa upasuaji pamoja na wenye kifafa cha mimba.
 Picha ya pamoja wafanyakazi wanawake wa benkiya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 picha ya pamoja.

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Adelphina Barongo akimkabidhi zawadi mteja wa akaunti ya Malkia, Erasmina Massawe ikiwa ni kwaajili ya kusheherekea siku ya mwanamke duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila Mwaka. 
 Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam akiwa na zawadi yake mara baada ya kuzawadiwa na Benki ya CRDB.
 Meneja huduma kwa wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Lilian Lema akimkabidhi mteja na Malkia wa benki hiyo, Victoria Fridoline zawadi kwaajili ya kusheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8.
 Meneja Msaidizi wa maendeleo ya Biashara wa benki ya CRDB tawi la Mlimani  City jijini Dar es Salaam, January Kirambata akimkabidhi mteja wa Malkia Akaunti ya malkia katika benki hiyo ikiwa ni kusheherekea siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
 Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Adelphina Barongo akizungumza na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake dunani ambayo hufanyika kila Mwaka Machi nane.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Adelphina Barongo akimkabidhi zawadi mteja wa tawi hilo na Malkia, Witnes Masawe ikiwa ni kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad