HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 7, 2018

AZAM FC, MWADUI HAPATOSHI KESHO CHAMAZI

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati AzamFC inatarajia kuwakaribisha wachimba madini wa Shinyanga Mwadui FC katika michuano inayoendelea ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Mtanange huo utakao ni wa ushindani kwa kila timu kutaka kupata ushindi utafanyika kesho saa moja usiku na mchezo utachezwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam FC wanatafuta alama 3 ili kuwakaribia Mabingwa watetezi Tanzania Bara  Yanga  wenye alama 40 wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Wakati Azam FC wakiwa nyuma kwa alama 35 na wapo nafasi ya tatu huku wakiongozwa na  vinara wa Ligi hiyo wekundu wa Msimbazi Simba  wakiwa na alama 46.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema kikosi kipo vizuri na wamejipanga kuchukua alama tatu wakiwa nyumbani.

"Tumeandaa timu vizuri na mwalimu  amepata muda wa kutosha wa kuandaa vijana  vizuri kuelekea mchezo huo na wachezaji wote walifanya mazoezi ya pamoja.

"Isipokuwa tutaendelea kumkosa mchezaji wetu katika mchezo wa kesho Yakubu Mohamed ambaye ni majeruhi"amesema Jaffary na kuongeza wanataka kubaki na alama tatu  kama ambavyo walizipata walipocheza na Singida United,"amesema Jaffary.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad