HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 February 2018

WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU WAKOSA SOKO LA UHAKIKA LA KUUZIA ZAO HILO

Na Jumbe Ismailly 
WAKULIMA wa zao la tumbaku katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, Mkoani Singida hawana soko la uhakika la kuuzia zao hilo kutokana na Makampuni yaliyokuwa yakinunua zao hilo kushindwa kuendelea kwa sababu ya madeni makubwa yanayovikabili vyama vya msingi vinavyolima tumbaku katika Halmashauri hiyo.
Afisa Maendeleo ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri hiyo Renatusi Mtatina aliyasema hayo kwenye mkutano maalumu wa Barazaa la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa ambaye alitaka kufahamishwa shilingi milioni 477 zitapatikanaji kwenye zao la tumbaku wakati serikali imeshusha ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi 3.
Aidha Mtatina alithibitisha kwamba ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri ya Itigi kwa mwaka huu bado haaijapata mnunuzi wa tumbaaku wala kampuni yeyote ile itakayonunua zao hilo na badala yake wakulima wataendelea kulima zao hilo na kwenda kuuza sehemu nyingine.
“Nia tunataraji kwamba watakuwepo wakulima ambao watalima lakini wanaweza wakauza sehemu nyingine lakini kwa Halmashauri ya Itigi hatujapata mnunuzi kwa hiyo patakuwa na changamoto kubwa katika kilimo cha tumbaku.”alisisitiza afisa huyo wa kilimo,umwagiliaji na ushirika.
Kwa mujibu wa Mtatina suala la matatizo ya vyama vya ushirika bado halijatatuliwa kwa sababu bado wana madeni makaubwa na ndiyo maana hawajapata mnunuzi wa zao hilo la tumbaku.
Katika swali lake la msingi,diwani wa kata ya Rungwa,Charles Machapaa alionyesha hofu ya kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri hiyo ya shilingi milioni 477 kutokana na serikali kushusha ushuru wa aina mbali mbali ya mazao,ikiwepo tumbaku,ushuru wa pamba pamoja na ushuru wa mazao mengineyo.
Kwa upande wake Mweka hazina wa Halmashauri hiyo,Charles Mnamba akitetea hoja hiyo alisisitiza kwamba katika msimu ujao uzalishaji wa kilimo cha zao la tumbaku utaongezeka zaidi ikilinganishwa na wa mwaka uliopita na utaweza kufidia kiwango cha ushuru wa asilimia mbili kilichopunguzwa na serikali.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni, Mkoani Singida, Ally Minja(wa pili kutoka kushoto) akiongoza mkutano maalumu wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele.
 Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, Yahaya Masare akichangia baadhi ya hoja kwa kutoa ufafanuzi kwa wajumbe wenzake wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni,Jumanne Ismaili akiwasilisha salamu za chama kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Itigi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kijiji cha Songambele,tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni Mkoani Singida wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kijiji cha Songambele, wakati wa mkutano maalumu wa baraza la madiwani.
Marobota ya tumbaku yaliyohifadhiwa kwenye moja ya ghala la chama cha Msingi Mitundu,tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni wakati wa uzinduzi wa soko la tumbaku lililofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Mitundu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad