HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 7 February 2018

WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUJIORODHESHA UHAMIAJI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewataka  wahamiaji walowezi kujiorodheshwa Marika ofisi zao za uhamiaji  wilaya.

Lengo ni kwamba baada ya kufanya hivyo watapewa vibali ya ukaazi vitavyofanya kuishi nchini kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu.

Hayo yamesemwa leo  jijini Dar es Salaam, Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima na kuwa uandikishaji wahamiaji walowezi ni la nchi nzima.

"Hivyo kwa wahamiaji walowezi lazima wajiorodheshe kwa kuwa na picha tatu za Paspoti zilizo katika wakati na wenye watoto wanatakiwa kuwa na picha tatu hizo", amesema.

Ameongeza kwa wale wataofanya hivyo watatambulika na kuendelea kuishi nchini bila kusumbuliwa kuhusu masuala ya uhamiaji na kutofautisha na wakimbizi na wahamiaji haramu.

Malima amesema wageni wote wanatakiwa kuitikia mwito huo wa Serikali pamoja na wale ambao wanaishi nchini na  kufanyakazi au biashara kinyume na sheria za nchi wanatakiwa kufika katika ofisi za wilaya ili  kuhalalisha ukaazi na kupewa vibali vinavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema  yeyote atakayejificha katika mchakato huo na baadaye kubainika anaishi kinyume cha cha sheria hatua kali zitachukuliwa.

Hatua hizo ni pamoja na kufukuzwa nchini mara moja au kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kukiuka sheria.

Aidha Malima amesema kuna matapeli wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaoingia nchini kwa kudai wao ni askari au maofisa wa uhamiaji na wakiwa hawana hata sare.

“Viongozi wetu wanajitahidi kwa kila hali kuitangaza nchi yetu na kuvutia wawekezaji sisi uhamiaji Dar es Salaam hatuwezi kukaa kimya na kuona hii ni nia njema ya Serikali inaharibiwa na watu wachache wasiotakia mema nchi yetu.
Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wahamiaji walowezi kujisajili ili kuweza kupatiwa vibali vya  kuishi nchini , leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad