HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2018

UTUMIAJI WA ISOTOPU ZA KINUKLIA KATIKA UTIBABU: VIPI INAWEZEKANA?

Kama kawaida maneno kama “kinuklia” au “mionzi” yanatisha ikiwa yanatumika katika nyanja za afya na maisha marefu. Hata hivyo, haiwezekani kufikiria utibabu za siku hizi bila ya teknolojia mpya inayotumia radioisotopu za kinuklia.
Duniani watu wanajua juu ya utumiaji wa mionzi na radioisotopu katika utibabu hasa kwa ajili ya utambuzi na utibabu ya magonjwa magumu mbali mbali. Katika nchi zilizoendelea, ambapo robo ya watu wote wa dunia wanaishi, mtu mmoja wa watu watano anatumia utibabu za utambuzi za kinuklia kila mwaka.
Lakini swali muhimu ni vipi dawa za kinuklia na radioisotopu (dawa zenye mionzi) zinafanya kazi na vipi zinaweza kuleta faida kwa Watanzania?
Kwanza, mionzi ni ufungaji wa nishati tu. Kama taa ya mwanga atomu za mionzi zinazalisha nishati inayotumika kwa ajili ya utibabu. Dawa za mionzi zinaingizwa katika mwili wa mgonjwa na sindano, kwa kumeza au kwa kuvuta pumzi.Ukubwa wa mionzi unaotumiwa ni mdogo sana. Mwilini radioisotopu zinatoa vyembe fupi (alpha au beta) ambavyo vinapoteza nishati yao yote katika umbali mfupi sana, kwa hivyo vinaathiri sana seli zilizoharibiwa. Kwa ujumla dawa za mionzi zinatumika kama matibabu: uharibifu wa seli za kansa, upungufu wa maumivu ya kansa ya mifupa na arthritis.
Kwa kutumia technolojia hizi za kinuklia wataalamu wa matibabu wanaweza kutambua na kutiba magonjwa mengi mbali mbali kwa njia salama na bila ya maumivu. Matibabu ya kinuklia yanawawezesha wataalamu kutambua kwa usahihi habarimbali mbali za afya ambazo hazipatikani kwa njia nyingine, zinahitaji upasaji au utumiaji wa kupima nyingine. Taratibu hizo zinatambua ukosefu ambapo ugonjwa unaendelea – mapema zaidi sana kabla ya testi za kawaida zinaweza kuutambua. Utambuzi mapema huo unawawezesha madaktari kuanza matibabu mapema zaidi, kwa hivyo tangazo zuri linawezekana.
Matibabu ya kinuklia inaweza kutambua magonjwa mengi mbali mbali. Yanatumika kwa kutambua mwilini vidonda visivyo vya kawaida bila ya upasuaji. Taratibu hizo pia zinapatia madaktari nafasi ya kutambua viungo vya mwili vikifanya kazi ipasavyo. Kwa mfano, matibabu ya kinuklia inaweza kutambua moyo ikipampu damu ipasavyo na bongo ikipata damu ya kutosha na kadhalika.
Utumiaji wa matibabu ya kinuklia si kitu kipya kabisa kwa Tanzania. Kwa kutumia teknolojia za kinuklia katika utibabu madaktari wenyeji wanafaulu zaidi katika utoaji wa utibabu mzuri kwa watu wenye magonjwa magumu kama kansa au magonjwa ya moyo na damu.
Mfano mzuri ni Ocean Road Cancer Institute (ORCI) mjini Dar es Salaam ambayo inatumia teknolojia ya kinuklia ya matibabu kama 3D scanning ili kutambua uvimbe na kuwatibu magonjwa bora zaidi. Kwa mfano kwa sababu ya mazingira na viwanda vya Dar es Salaam na maeneo yaliyopo karibu mji wenyeji wengi zaidi wanaumwa na kansa. Lakini pia watu wengi zaidi wanaweza kuitambua kansa kwa sababu ya nafasi ya hospitali jijini.
Data ya ORCI inaonyesha kuwa katika Dar es Salaam asilimia 17 za wagonjwa wa kansa wanatambuliwa, asilimia 11 katika Mbeya na Morogoro na asilimia 9 katika Kilimanjaro.
Dr Hamid Mustafa ambaye ni daktari wa kansa katika Regency Specialized Polyclinic katika Dar es Salaam anasisitiza kuwa nafasi za kuvumbua na kuangalia kansa zinaongeza namba ya kesi za kansa zilizotambuliwa. Na bila ya nafasi hizo wagonjwa hao hawangepata matibabu kabisa.
Mwaka 2017 mkurugenzi naibu wa ORCI Dr Julius Mwaisegale alieleza kuwa kesi za kansa zilizotambuliwa katika ORCI ziliongezeka toka kesi 2,500 mpaka 56,000 katika muda wa miaka 2005 mpaka 2015. Utumiaji wa matibabu ya kinuklia ni muhimu sana kwa nchi ili kutambua na kutibu magonjwa magumu mapema zaidi. 
Tanzania inalenga kuanzisha usajili wa kansa kama hatua moja ya siasa mpya ya uongozi wa magonjwa yasiyo ya mawasiliano.Uborefu wa nafasi za matibabu ya kinuklia itasaidia kupunguza kiwango cha kifo kwa sababu ya kansa kwa sababu utambuzi wa magonja mapema zaidi utayaokoa maelfu ya maisha.
Siku ijayo Tanzania inaweza kufuata mfano wa Zambia ambayo inapanga kuanzisha kituo chake cha sayansi na teknolojia ya kinuklia ili kuunga mkono sekta ya kinuklia yake yenyewe. Kituo hakitazalisha isotopu ya matibabu tu lakini pia itawapatia wataalumu nafasi za utafiti sahihi katika nyanja ya kinuklia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad