Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza promosheni mpya inayokwenda kwa jina la Nyaka Nyaka ambayo itawawezesha wateja wa Tigo watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya
*147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi
ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Wengine pichani ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik
Boudiaf pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza promosheni mpya inayokwenda kwa
jina la Nyaka Nyaka ambayo itawawezesha wateja wa Tigo watakaonunua
bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya
*147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa
matumizi
ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali
Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni murwa kwa wateja wake wote
watakaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya
*147*00#, ambapo watapokea bonasi ya hadi 1GB bure papo kwa hapo kwa matumizi
ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter.
Pamoja na haya, wateja hao pia watapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja
zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zaidi ya elfu moja ambazo zinatolewa na Tigo
katika promosheni hiyo kabambe ya ‘Nyaka Nyaka Bonus’.
Akitangaza ofa hizo jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Tarik
Boudiaf alisema kuwa ofa hizo murwa ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaolenga
kukutana na mahitaji ya wateja na kuwezesha kila mtu afurahie huduma za kidigitali
katika mtandao ulioboreshwa wa Tigo.
“Kupitia mtandao wetu mathubuti wa 4G wateja wetu tayari wanafurahia huduma bora
zaidi za intaneti. Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inatoa fursa kubwa kwa wateja
wengi zaidi kumiliki simu janja zenye uwezo wa 4G na kupokea bonasi kubwa za data
zitakazowawezesha kuwa sehemu ya mageuzi makubwa ya kidigitali yanayoongozwa
na Tigo,’ alisema.
Tigo ndio mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake ambapo katika soko la
simu za mkononi nchini, ni wateja wa Tigo pekee wanaopokea bonasi za bure kwa kila
kifurushi wanachonunua. Tigo pia imejizolea umaarufu mkubwa kwa promosheni zake
bunifu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kupitia
promosheni mpya ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inalenga kuongeza matumizi ya data
pamoja na kuongeza matumizi ya simu janja za kisasa (Smartphone) nchini, hivyo
kuisogeza Tanzania hatua moja mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali.
‘Tunafahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma za
mtandao na ndio maana Tigo inazidi kuwekeza katika kupanua na kuboresha huduma
zake za mtandao.
Kupitia promosheni hii tunalenga kuongeza idadi ya watumiaji wa
simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini,’ alisema.
“Tunawakaribisha wateja wetu wote kuchangamkia fursa hii kwa kununua vifurushi vya
data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00# ili waweze kufaidi bonasi
za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya mitandao ya jamii kama vile Facebook,
WhatsApp, Instagram ama Twitter.
Vile vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza
katika droo ambapo watapata nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja
1,000 aina ya TECNO R6 yenye uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,”
Tarik alisisitiza.
No comments:
Post a Comment