HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 5, 2018

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAZISHI YA MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Wajukuu wa marehemu pamoja na wafiwa wengine wakiwa katika hali ya majonzi makaburini hapo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi  la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad