HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 2, 2018

MWANANCHI MWENYE ULEMAVU YUSUF ABDULRAHMAN NDEMANGA AKABIDHIWA BAJAJI ALIYOAHIDIWA NA RAIS MAGUFULI

 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa wakimwongoza mlemavu wa maungo Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga kwenye Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018.
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi  mlemavu wa maungo  Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. Kulia ni ke w Bw. Ndemanga, Bi. Hawa Mohamed.

  Mlemavu wa maungo  Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga na mkewe Hawa Mohamed Wakiondoka na Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Abdulrahman Ndemanga ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam Agosti 25, mwaka jana. Bw. Ndemanga alimuomba Rais msada wa kupatiwa Bajaji ili ajimudu kiusafiri na kiuchumi.

Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad