HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 20 February 2018

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA MBALIMBALI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA UGANDA

Makatibu  Wakuu na Wataalam wa Wizara mbalimbali kutoka nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan ya Kusini wamekutana nchini Uganda ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo. 

Katika kikao kilichofanyika  Kampala nchini Uganda, Makatibu Wakuu hao na wataalam walijadili ripoti kuhusu  masuala ya Biashara, Fedha, Ushuru, Siasa, Miundombinu na Afya iliyokabidhiwa katika kikao cha Mawaziri wa Jumuiya hiyo kilichofanyika kuanzia tarehe 19 na kitahitimishwa tarehe 21 Februari, 2018.

Wizara kutoka Tanzania zilizohudhuria kikao hicho ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,  Wizara ya Katiba na Sheria, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Wazee Jinsia na Watoto na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.
Wizara ya Nishati  iliwakilishwa na Katibu Mkuu, Dkt Hamis Mwinyimvua aliyeambatana na Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga,  Mjiolojia Mkuu, Adam Zuberi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Edith Mwanje ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha Makatibu Wakuu na Watalaam kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akizungumza katika kikao hicho.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kulia waliokaa) akiwa katika kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalam ambao wamehudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda wa pili kulia  ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju, wa tatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Stephen Mbundi katika Wizara ya Mambo ya Nje, wa nne kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga.
 Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wataalam kutoka Nchi wanachama husika na Wajumbe mbalimbali wakijadili ripoti itakayotumika katika Mkutano wa 35 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri ambao unafanyika tarehe 19– 21 Februari, 2018 mjini Kampala nchini Uganda.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Shomar O. Shomar (mbele), Kaimu Kamishna Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (mstari wa nyuma, kushoto) Mtalaam kutoka Wizara ya Nishati, Adam Zuberi na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Clarence Ichwekeleza wakiwa katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Mbundi wakifuatilia mada katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad