HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 3 February 2018

IMETOSHA YASHIRIKI SIKU YA KANSA DUNIANI KWA KUPIMA WATOTO WENYE UALBINO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Imetosha, Henry Mdimu amesema kuwa watoto wenye ualbino kati watano  hadi saba wanafariki kwa mwezi  katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na Kansa ya ngozi.

Mdimu ameyasema hayo  wakati wa upimaji wa kansa kwa watoto wenye ualbino katika Hospitali ya  0cean Road katika Maadhimisho ya Siku ya Kansa Duniani  ambayo huadhimishwa Februari 3 kila mwaka.

Amesema  kambi ya upimaji huo wameshirikiana na Hospitali ya Ocean Road na Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS)  katika kuhakikisha kila mtoto mwenye ualbino anapata vipimo.

Amesema kambi ya upimaji hiyo itaendelea  mikoani ambayo watapima madaktari wa Ocean Road ili kujua hali ya tatizo  ya Kansa kwa watoto wenye Ualbino na baada ya kupimwa na kuonekana kuanza kupatiwa matibabu.

“Mimi Mkurugenzi wa Imetosha naona nina wajibu wa kuwa moja kwa moja na watu wenye ualbino kuhakikisha maisha ya watoto yanaokolewa nikifanya mimi na mwingine atafanya”amesema Mdimu.


Mkurugenzi Mtendaji wa Imetosha, Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Kansa Duniani ambayo Taasisi ya Imetosha imeratibu upimaji wa watoto leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiandisha  kwa ajili ya upimaji katika Hospitali ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watu wenye ualbino wakiwa  wamekaa  kwa ajili ya kwenda kupata taraibu za upimaji katika Ocean Road leo jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii )

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad