HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 February 2018

DIAMOND NA HAMISA WAMALIZA TOFAUTI ZAO


Na Karama Kenyunko , Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul “Diamond Platzum” mapema leo asubuhi amefika katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Ustawi wa Jamii kwenye mahakama ya watoto kwa ajili ya usuluhishi juu ya matunzo ya mtoto wake aliyezaa na mlimbwende Hamisa Mobeto.

Alianza kuingia Diamond akafuatiwa na Hamisa baada ya muda kidogo ambapo walikaa kwa zaidi ya saa moja.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza usuluhushi huo, Diamond alisema,
 
“Kiasi cha pesa tunavyoviandika kama kama hivi, tunazungumza tu, lakini watoto hawahitaji mahitaji mengi, wakati mwingine mtoto wako una uwezo wa kumpa hadi Shilingi milioni 100 na huwezi kusema simpi kwa sababu niliandikisha nitampa Laki Moja haimsaidii”.

Alisema wao kama wazazi wameweka mazingira mazuri ya kumlea mtoto wao kwa kadri ya uwezo wataokapata, kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora wakipata watakula nae wakikosa watalala

“Nyuma ya stori hii nimejifunza kwamba siyo kila mtoto ambaye haishi na baba au mama yake basi asiyeishi nae anatatizo nae, hata mi nimejifunza pia kwa mimi na baba yangu,kuna vitu wazazi wanavifanya vinakuwa siyo fresh,vinatengeneza story, mtoto baadae akikua hajui story ya nyuma anajua mzazi mmoja anamatizo akajua dingi noma lakini siyo tu”.

Aidha Diamond amesema ni vema wazazi wote wawili watumie busara kuangalia namna gani wanasuluhisha ugomvi hasa hasa pale wanapokuwa wameitilafiana, watumie busara kutafuta njia ya kusuluhisha bila kuwaumiza watoto

"Nitahakikisha mtoto wangu akue katika mazingira mazuri, asome kadri ya uwezo nitakaokuwa nao, kwani maisha ni kupanda na kushuka kuna wakati unakuwa hauna unasema leo mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha ndivyo yalivyo amesema Diamond.

Amesema, “Kiumakini hakukuwa na vita kati yetu sisi wawili, ila kwa upande wa mwenzangu kulikuwa na watu wanaingiza chuki ilimradi kutengeneza mazingira ya kumkomoa Diamond kitu ambacho tumeona hakimsaidii mtoto.

“Tumekubaliana na tumeyamaliza na tumeweka misingi mizuri ya kumlea mtoto wetu, kwani mwisho wa siku hata mahakama haiwezi kunambia nimlipe Milioni 5 nitaitoa wapi, nina kazi mie, Mahakama imenipa kazi au kuna mtu amenipa kazi...? au eti mtoto umjengee nyumba, ulinipa mie nyumba alisema Diamond.

Alipohojiwa baada ya kumalizika kwa usuluhishi, wakili wa Hamisa Mobeto,Walter Goodluck amesema, "leo tulikuja kwa usuluhishi na wamesuluhishwa Ila sasa wamesuluhishwa nini na nini hilo tutalijua badae", amesema

Novemba 10, mwaka jana na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo upande wa watoto ya watoto, Devotha Kisoka, aliitupilia mbali kesi aliyofunguliwa Mobeto juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul kwa kuwa ilifunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.

Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine akiiomba matunzo ya mtoto.

Pia alikuwa akiiomba mahakama imuamuru Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akifika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto.
Hamisa Mobeto akiwa kwenye mahakamani kisutu leo
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka ustawi wa jimii kwa ajili ya kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad