HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 9, 2018

ALIYEKUWA KAMISHINA MADINI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Ally Samaje amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za Matumizi mabaya ya madara.

Mwendesha Mashtaka wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai amedai, mshtakiwa Samaje ambaye pia alikuwa Katibu wa Bodi ya umUshauri wa Madini, ametenda kosa la kwanza kati ya Aprili 9 na June 21, mwaka 2013.

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa kuwa, mshtakiwa Samaje akiwa katika utendaji wa kazi zake alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuitisha mkutano wa hiyo bodi na kupata ushauri wake kwa kuzingatia maombi ya leseni ya madini Namba HQ-P26114 kwa ajili ya (Gamestone and Associated minerals) yakiwamo madini ya Graphite na Marble katika eneo la Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoa Wa Manyara.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa maombi hayo yaliwasilishwa na Kampuni ya Tanzanite one mining ltd na State mining Corporation.

 Kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha sheria ya madini no. 14 ya mwaka 2010  kwa lengo la kuipatia faida kampuni hizi kwa kupata eneo la madini ambalo ni kilometa 7.6.

Katika shtaka la pili, Swai alidai kuwa Aprili 16 mwaka 2013 mshtakiwa Samaje alitumia vibaya madaraka yake kwa kutoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa leseni na Haki za Madini John Nayopa kuandaa leseni kuchimba madini ya Gemstones ikiwamo Tanzabite,Graphite na Marble bila ya kuzingatia mfumo wa uendeshaji wa taarifa za madini wa Cadastie (MCIMS) wa Wizara ya Nishati na Madini wa eneo la kilometa 7.6 lililopo Mererani wilaya  Simanjiro.

Ilidaiwa kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 49(2)(b) cha sheria ya madini namba 14 ya 2010 na kusababisha kampuni hizo kupata faida ya leseni  za kuchimba madini.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama ilimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye anuani zinazojulikana watakaosaini bondi ya milioni 50.

Kesi imeahirishwa hadi Februari  28 mwaka huu,

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad