HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 19 January 2018

WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO ZINGATIENI SHERIA- NDITIYE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema watoa huduma za mawasiliano nchini lazima wafuate sheria zilizowekwa ili kutoa huduma bora za mawasiliano kwa walaji.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bdhaa za mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)wakati wa mkutano wa wadau jijini Dar es Salaam.

Amesema TCRA isiache kuwachukulia hatua watoa huduma wanaokwenda kinyume na sheria za leseni ya utoaji wa huduma za mawasiliano nchini. Amefanunua kitabu cha mwongozo kinatoa elimu kuhusu kutatua cha changamoto za mawasiliano na njia za kufuata pale wanapoona taarifa tofauti katika matumizi ya mawasiliano.

Kwa upande wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa teknolojia kumefanya kwenda kisasa tofauti na miaka ya nyuma .

Amesema katika tekonolojia ya Tehama wajasiriamali wengi wanaitumia katika kujiingizia kipato ambapo lazima watoe maudhui yanayoendana katika sheria zilizowekwa. MKurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mwongozo uliopo katika kitabu hicho utasaidia kutatua changamoto za mawasiliano kwa watumiaji kujua njia za kufuata pindi wanapoona taarifa tofauti.
 Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza katika uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kuhusu sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba akitoa taarifa za uandaji wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano na sekta ya utangazaji , leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa,Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye wakiwa wameshika vitabu kuashiria uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, jijini Dar es Salaam.
 Msanii Mrisho Mpoto maarufu Mjomba akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa  kitabu cha mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano , leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad