HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 19 January 2018

MTANDAO WA KIJAMII WAJITOLEA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii
MTANDAO wa kijamii wa kuutangaza utalii wa Deiplaces umesema umejipanga vema kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Deiplaces Dk.Paul Bamutaze amesema kwa kutumia mtandao huo watakuwa wakitoa taarifa mbalimbali zinazohusu utalii wa Tanzania ambapo taarifa hizo zitasomwa na watu wa mataifa mbalimbali duniani.

Amesema wanatambua juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuutangaza utalii pamoja na vivutio vilivyopo lakini nao wameona ipo haja ya kusaidia kutangaza utalii uliopo nchini Tanzania.

"Tumekuja Tanzania kwa ajili ya kuanzisha mtandao wa kijamii ambao utakuwa ukihusika na utoaji taarifa sahihi zinazohusu utalii na vivutio vilivyopo. Lengo letu ni kufanikisha kila anayetaka kufahamu kuhusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii basi apate kutoka kwetu.

"Pia mtandao huu utakuwa sehemu sahihi ya hata vyombo vya habari ambavyo vinataka kupata habari sahihi zinazohusu utalii basi watazikuta kwetu.

"Hakutakuwa na gharama yoyote unapotaka kupitia taarifa za utalii ambazo tunakuwa tunaziweka,"amesema. Dk.Bamutaze amefafanua unapotaka kuzungumzia Mlima wa Kilimanjaro hakuna ambaye hajui historia yake, na hivyo wao watakapoamua kutoa habari za mlima huo watajikita kuelezea maisha ya watu wanaouzunguka mlima huo pamoja na mazingira yake.

Amesema unapotaka kuizingumzia mbuga ya Serengeti ambayo ina kila aina ya vivutio vya utalii basi lazima taarifa ziwe zenye ukweli na si za kupotosha. Amefafanua wamekuwa wakitangaza utalii wa nchi mbalimbali za Afrika na sasa wanataka kujikita Tanzania.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa deiplaces Dk.Paul Bamutaze akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad