HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 17 January 2018

WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Elimu Solutions (T) Limited Neithan Suedy amesema ni vema Watanzania hasa wanafunzi nchini kuwa makini na matapeli wanaochukua fedha za wanafunzi kwa kigezo cha kuwatafutia vyuo vikuu nje ya nchi. 

Amesema wanaungana na Balozi wa Tanzania nchini China kuonya tabia ya baadhi ya mawakala kuchukua fedha za wanafunzi na kisha kushindwa kuwapeleka Kwenye vyuo ambavyo wanaahidi kuwapeleka au kuwapeleka na kusababisha wanafunzi wakifika huko kukosa malazi na makazi. 

Akizungumza Dar es Salaam leo, Sissy amesema wenye tabia hiyo wanasababisha matatizo kwa wanafunzi na wanaokwenda huko nchini China wanasababisha mzigo kwa vyuo husika.

"Wanafunzi wanatapeliwa sana na watu hao ambao wanajiita mawakala wa kutafutia ufadhili wanafunzi wa Tanzania kwa vyuo vikuu vya nchini China. 

"Ni vema Serikali yetu ikasaidia kudhibiti utapeli huu ambao unafanywa kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nchini China, "amesema Suedy. 

Akizungumzia kwa upande wao amesema wamekuwa wakitafuta ufadhili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiendeleza kielimu nchini China na wanachozingatia wao ni kufuata taratibu ambazo zinatambulika kisheria. 

Pia amesema ambacho wao wanakifanya ni kutafuta vyuo vinavyotoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na kisha wanafanya udahili na wale ambao watakidhi vigezo na sifa wanawaunganisha na vyuo vikuu husika vilivyopo nchini China. 

"Hatuchui ada ya mwanafunzi yoyote yule.Jukumu letu ni kutafuta vyuo vikuu na kisha mwanafunzi kulipa gharama zote chuo kikuu husika. 
"Sisi tunachukua gharama tu ambayo inatokana na mchakato wa kutafuta ufadhili kwa wanafunzi wanaokwenda huko, "amesema Suedy. 

Pia ameelezea namna ambavyo Elimu Solutions (T) Limited wanafanya udahili kwa wanafunzi wanaohitaji ufadhili kwa vyuo vikuu vilivyopo China, Japan na South Korea amesema mbali ya kufanya udahili katika ofisi zao pia wameanzisha utaratibu wa kudahili wanafunzi kwa njia ya mtandao. 

Amesema udahili kwa njia ya mtandao unafanyika kwa kutumia WWW.elimusolutions.co.tz ambako anayehitaji akishaingia atakutana na maelekezo ambayo yatamuwezesha kudahiliwa

Amesema kwa mwaka huu watakuwa na udahili wa wanafunzi Machi,Julai na Septemba na waombaji ni wenye elimu ya ngazi ya  digrii na mastars.

Amesema na watakuwa wakifanya udahili kwa mujibu ratiba ambao wenye digrii watafanyiwa udahili kwa awamu ya kwanza Machi, Julai na Septemba na wenye mastars idahili utafanyika Juni mwaka Juni. 

Amesema Elimu Solutions (T) Limited ni mawakala rafiki wa kisheria wa vyuo vikuu zaidi 300 kutoka nchini China, Japan na Korea Kusini. 

Amesema kutokana na mahusiano hayo wameweza kuhakikishiwa kupata nafasi zaidi ya 1500 za masomo (scholarship)kwa kila muhula mpya wa masomo na kwa kila ngazi ya masomo kutoka Kwenye vyuo vyao washirika. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Tanzania Ltd, Neithan Swedy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa zoezi la kutuma maombi ya udahili wa masomo kwa wanafunzi wa nje ya nchi (China, Japan na Korea Kusini) pamoja na taratibu mbalimbali zinazopaswa kuzingatiwa na waombaji. Kushoto ni Afisa Tawala wa Taasisi hiyo, Irene Kigwangwa  leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Ltd, Neithan Swedy akionyesha kwa waandishi wa habari nyaraka ya Namba ya Utambulisho Mlipa Kodi (TIN) inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) na kupaswa kuwa nayo kila kampuni ya uwakala wa utafutaji wa nafasi za masomo katika vyuo vya nchi za nje ya Tanzania. Wengine ni Afisa Tawala Irene Kigwanga na Meneja mwendeshaji wa Elimu Solutions, Ibrahim Swedy leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad