HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2018

VYAMA VYA SIASA VYAKUMBUSHWA KUTII SHERIA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevikumbusha vyama vya siasa kutii Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za uchaguzi na kanuni zake wakati wa uchaguzi.

Wito huo umetolewa kupitia barua aliyoviandikia vyama vya siasa yenye kumbukumbu HA.322/362/01/165 ya tarehe 30 Januari, 2018.

“ Natambua kuwa baadhi ya vyama vyenu vinashiriki katika chaguzi ndogo za Ubunge na Udiwani zinazoendelea katika majimbo na kata.  Hivyo, natumia fursa hii pia kuvipongeza vyama vyote vinavyoshiriki katika chaguzi hizo, kwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kidemokrasia. Aidha, naviasa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kuheshimu na kufuata sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kanuni zake, kwa kuepuka vitendo vya fujo na lugha za matusi na uchochezi” imenukuliwa barua hiyo.

Jaji Mutungi pia ametoa wito kwa mwanachama wa chama chochote cha siasa au chama kinachoshiriki uchaguzi kutoa taarifa katika mamlaka husika kuliko kujichukulia sheria mkononi, endapo kitashuhudia kwa kuona ama kusikia uvunjifu wa Sheria unaohusu chaguzi zinazofanyika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad