HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 10 January 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZINDUA STUDIO MPYA ZA ZBC ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya ZBC mnazi mmoja kwa ajili ya Uzinduzi wa Studio ya Kisasa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Studio ya Kisasa ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ikiwa ni shamra shamra za sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 54.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC Aiman Duwe akitowa maelezo wakati wa kutembelea Studio ya kurikodia baada ya uzinduzi huo, uliofanyika katika jengo la ZBC mnazi mmoja Zanzibar leo.9-1-2018.
MOJA ya Studio Mpya za kufanyia mahojia na vipindi iliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Digital Video International. Geal Lancrenon, akitowa maelezi wakati wa uzinduzi huo wa Studio Mpya za ZBC kampuni yake imesimamia ufungaji wake.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan King akitowa maelezo ya vifaa vipya vilivyofungwa katika Studio hizo wakati wa ufunguzi wake uliofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza wakiwa katika Studio ya kurikodia katika jengo la ZBC.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mfanyakazi wa ZBC Chumba cha kurushia matangazo ya ZBC Fatma Abubakari akitowa maelezo jinsi ya urushaji wa picha wakati wa ufunguzi wa Studio Mpya za ZBC uliofanyika leo katika jengo lao Mnazi Mmoja Zanzibar.
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Aiman Duwe akitowa maelezo ya picha za mitambuo mbalimbali ya Studio hizo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akitembelea jengo hilo kujionea mitambo hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mfanyakazi wa ZBC Maimuna Said, akitowa maelezi jinsi ya kurusha matangazo kutoka chumba cha Wageni Maarufu (VIP) wakati wa kufanya mahijiano.


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC ) Aiman Duwe, akifanya mahojiano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya uzinduzi wa Studio Mpya za ZBC Mnazi mmoja Zanzibar, ikiwa ni ktika shamrashamra za kutimia miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Studio Mpya za Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) mnazi mmoja Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad