HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 26 January 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA SHARJAH.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya moja ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Sharjah  na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Abdalla Eleweis. Moja ya bidhaa aina ya juice ya matunda inayotengenezwa na kiwanda hicho.(Picha na Ikulu)
 MKURUGENZI Mkuu wa Kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Abdallah Eleweis akitowa maelezo ya kiwanda chake na bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) (Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Sharjah, Abdallah Eleweis na Balozi Mdogo wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu anayefanyia kazi Dubai,Ali Jabir Mwadini, wakifuatilia maelezo ya kitaalamu ya ufungaji wa Ngombe wa maziwa yakitolewa na Meneja Mkuu wa kiwanda cha maziwa cha Al Rawabi Sharjah (Picha na Ikulu)
 MENEJA Mkuu wa Shamba la Ngombe Dr. Ahmed Eltigani A.Rahim Al Mansour akitowa maelezo ya kitaalamu ya ufungaji wa ngombe wa maziwa wanaofungwa na kampuni ya Al Rawabi Sharjah kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein na viongozi wengine wakifuatilia maelezo ya kitaalamu yakitolewa na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Sharjah Dr. Ahmed Altigani akiwasilisha ufungaji bora wa Ngombe wa maziwa.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib akiuliza swali kuhusiana na utaalamu wa ufugaji bora wa ngombe wa maziwa wakati wa hafla hiyo katika kiwanda cha maziwa cha Al Rawabi Sharjah.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dk. Khalid Salum Mohammed alipata fursa ya kuuliza swali wakati wa kuwasilisha ufungaji bora wa ngombe wa maziwa wanaofungwa na Kiwanda cha maziwa Al Rawabi Sharjah.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Sharjah  Abdallah Eleweis,baada ya hafla hiyo ya kutembelea kiwanda hicho.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Senior Vice President – Commercial Services Atiq Juma Faraj Nasib, baada ya hafla hiyo ya kutembelea kiwanda cha maziwa.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya ngombe wa maziwa wakiwa katika sehemu yao kwa ajili ya ukamuaji wa kwa kutumia mashine maalumu, zinazotumika kwa ukamuaji wa maziwa katika kiwanda hicho hicho cha Al Rawabi Sharjah.(Picha na Ikulu)
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Maziwa cha Al Rawabi Sharjah Abdallah Eleweis, akitowa maelezo kwa Rais walipotembelea mabanda ya ngombe wa kisasa huzaliwa lita 60 kwa ngombe mmoja. Akiwa katika ziara yake. (Picha na Ikulu)  
BAADHI ya Ngombe wa kisasa wa maziwa wakiwa katika maeneo yao ya malisho katika kiwanda cha maziwa cha Al Rawabi Sharjah.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad