HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 January 2018

RAIS MAGUFULI AMEMTEUA ALIYEKUWA KATIBU MKUU IKULU, BW. ALPHAYO KIDATA KUWA BALOZI

Rais John Magufuli ameteua mabalozi wapya wawili ambao ni Alphayo Kidata na Meja Jenerali Mstaafu, Simoni Mumwi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa Kidata umeanza jana Jumatano Januari 10.

Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad