HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 30, 2018

Necta yatangaza matokeo ya kidato nne

*Philison Mdee aongoza kwa wavulana,  Ellizabeth  Mangu aongoza wasichana

*Wengine 265 matokeo yafutwa, yumo aliyeandika matusi kwenye majibu


 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHULE ya Sekondari ya St.Francis Girls imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017.

Akitangaza  sekondari ambazo zimeshika nafasi za juu kwenye matokeo hayo, leo jijijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk.Charles Msonde amesema nafasi ya pili imechukuliwa na sekondari ya Feza Boys na nafasi ya tatu sekondari ya Kemebos.

Wakati nafasi ya nne imeshikiliwa na sekondari ya  Bethel Saabs Girls, nafasi ya tano sekondari ya Anuarite, nafasi ya sita sekondari ya  Marian Gilrs huku nafasi ya saba ikishikiliwa na sekondari ya Canossa, wakati nafasi ya nane imechukuliwa na sekondari ya Feza Girls, nafasi ya tisa sekondari ya Marian Boys na nafasi ya 10 sekondari ya Shamsiye Boys

WALIOONGOZA 10 BORA KITAIFA
Kwa upande wa wanafunzi ambao wameshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi kitaifa kwenye matokeo hayo, Dk.Msonde alisema nafasi ya  kwanza imeshikwa na mwanafunzi Philison Mdee(Marian Boys), wakati nafasi ya pili imeshikwa na Eliza Mangu(Marian Girls), nafasi ya tatu
Ana Mshana(Marian Girls)

Ametaja nafasi ya nne imeshikwa na Emanuel Makoye(Ilboru), nafasi ya tano Lukelo Luoga(Ilboru), nafasi ya sita Fuad Thabit(Feza Boys), nafasi ya saba Godfrey Mwakatage(Uwata), nafasi ya nane Baraka Mohamed(Angeles), nafasi ya tisa Lilian Moses(Marian Girls) na nafasi ya kumi kitaifa imechukuliwa na Everine Mlowe(St. Francis Gr)

WAVULANA 10 BORA KITAIFA 
Akitangaza walioshika nafasi ya kwanza hadi ya 10 kitaifa kwa mujibu wa Dk.Msonde ni Philison Mdee(Marian Boys), nafasi ya pili Lameck Makoye(Ilboru), nafasi ya tatu Tadei Luoga(Ilboru), nafasi ya nne Fuad Thabit (Feza Boys).

Wakati nafasi ya tano ni  Godfrey Mwakatage(Uwata),nafasi ya sita  Baraka Mohamed(Angeles),nafasi ya saba  Noel Shimba(Marian Boys), nafasi ya nane ni Patrick Robert(Mzumbe), nafasi ya tisa Robison Eliona(ILboru) na nafasi ya 10 bora kitaifa imechukuliwa na mwanafunzi Harrison Simkoko (Mzumbe)

WASICHANA 10 BORA KITAIFA
Dk.Msonde ametaja wasichana walioongoza kwenye matokeo ya mtihani huo ambapo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Ellizabeth  Mangu(Marian Girls) nafasi ya pili Anna Benjamin Mshana(Marian Girls), watatu ni Lilian Moses Katabalo(Marian Girls) na nafasi ya nne ni Eveline Edward Mloe(St.Francis Girls).

Nafasi ya tano imechukuliwa na Rosemary Godfrey Ritth (St.Francis), nafasi ya sita ni Priscilla Hermenegild Kiyagi(St.Francis) nafasi ya saba ni Comfort Aloyce Mkangaa (St.Francis), nafasi ya nane Reginelly Gaudence Moshi(Kifungilo Girls) nafasi ya tisa Maria Hewa Gambaloya(Mariam Girls) na nafasi ya 10 ni Dorice Humphrey Shadrack(St.Francic)

UFAULU WAONGEZEKA KWA ASILIMIA SABA

Akizungumzia matokeo hayo, Dk.Msonde amefafanua kuwa ufaulu umeogezeka kwa asilimia saba na kwamba jumla ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017.

Ameongeza kati yao watahiniwa  287,713 sawa na asilimia 77.09 wamefaulu na kati yao wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana ni 143,985 sawa na asilimia 79.06.

"Mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.Matokeo ya watahiniwa 50 wa shule waliopata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu,"amesema Dk.Msonde.

Ameeleza pia NECTA imeamua kufuta matokeo ya watahiniwa 265 ambao wamebainika kufanya udanganyifu wakati wakifanya mtihani huo."Kuna mmoja ya mtihani tumekuta mtahiniwa ameandika matusi kwenye haratasi ya majibu,"amesema Dk.Msonde.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad