HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 10, 2018

NEC yatangaza uchaguzi mdogo wa madiwani

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nyingine sita utafanyika Februari 17 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage alisema jana kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalibali zikiwemo kifo na baadhi ya madiwani kujiuzulu.
Alizitaja kata ambazo zitafanya uchaguzi huo mdogo kuwa ni Kata ya Buhangaza iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Kata ya Kanyelele iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kata ya Mitunduruni iliyoko katika Manispaa ya Singida.
Kata zingine ambazo zitafanya uchaguzi ni kata ya Kashashi, Gararagua na Donyomuruak ambazo madiwani wake wamejiuzulu hivi karibuni.
“Napenda kutumia nafasi hii kutoa tarifa kwa umma kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hizo februari 17, 2018,”alisema Jaji Kaijage.
Uchaguzi huo unafanyika sambamba na uchaguzi mwingine mdogo wa wabunge ambao utafanyika katika majimbo mawili ya Songea Mjini ambako mbunge alifariki na Longido mbunge wake alivuliwa ubunge na mahakama.
Aliongeza kuwa kutokana na uchaguzi huo mdogo, ratiba ya uchaguzi huo itaanza tarehe 18 hadi 24 Januari ambako tume itatoa fumu za uteuzi, uteuzi wa wagombea utafanyika januari 24 na kampeni zitaanza Januari 25 hadi Februari 16 na uchaguzi wenyewe utafanyika Febuari 17.
Kaijage alitoa mwito kwa vyama vya siasa, wadau wa uchaguzi na wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo.
“Tume inaviasa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya katiba, sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, kanuni za uchaguzi na serikiali za mtiaa za mwaka 2015, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo yaliyotolewa na tume katika kipindi chote cha uchaguzi mdogo,”alisema Jaji Kaijange.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad