HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 13 January 2018

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.  
Akihutubia katika mkutano wake kwa wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.
Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wao wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad