HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 29, 2018

NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AKUTANA NA UGENI KUTOKA NCHINI MAREKANI

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akimkaribisha katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley, kabla ya kuanza mazungumzo kwa ajili ya ugeni kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.  Katikati ni Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Rendi Mccoy aliyetembelea Wizara hiyo kwa ajili ya kuona Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu pamoja na kuangalia ni jinsi gani Marekani inaweza ikasaidia katika kukabiliana na vita hiyo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) akiwafafanulia jambo, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Rendi Mccoy (wapili kushoto), na Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley (kushoto), wakati wa mazungumzo na maafisa hao yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Maafisa hao kutoka Marekani wamefika wizarani hapo kwa ajili ya kuona jinsi Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu pamoja na kuangalia ni jinsi gani Marekani inaweza ikasaidia katika kukabiliana na vita hiyo. Kulia ni Selectine Makoba, Afisa kutoka Ofisi ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akimsikiliza Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Rendi Mccoy (katikati), wakati alipokua anafafanua jambo baada ya kupewa taarifa ya jinsi Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu. Ugeni huo kutoka Marekani pia uliangalia jinsi gani nchi hiyo inaweza ikaisaidia Tanzania katika kukabiliana na vita hiyo. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad