HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 29 January 2018

DC MLOZI AHIMIZA WATENDAJI NA MADIWANI WA MANISPAA YA TABORA KUZINGATIA MUDA.

Na Tiganya Vincent

MKUU wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi amewataka Madiwani na Watumishi wa Manispaa ya Tabora kuzingatia muda wanapokuwa katika shughuli mbalimbali kama wanataka kupata maendeleo ya haraka.

Queen alitoa hiyo jana mjini hapa baada ya kukwera baadhi ya watumishi na Madiwani wa Manispaa ya Tabora kuchelewa kuingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza Maalumu la Madiwani lilikuwa likipitia rasmu ya mpango wa bajeti ya mwaka ujao.

Alisema kuwa hatua hiyo baadhi ya watumishi na madiwani kuchelewa kulisababisha Kikao hicho kichelewe kuanza na hivyo kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Queen alisema kuwa wakiendelea na mwendeo huo watasababisha Manispaa hiyo kupitia na Halmashauri nyingine kimaendeleo na hawataweza kwenda na kasi ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Naomba nieleze kusikitishwa kwangu kwa ucheleweji huo wa kuanza vikao…nimefika hapa saa 3.00 asubuhi nikitarajia ndio muda wa kikao kuanza lakini hadi hivi sasa saa 5.00 asubuhi ndio tunaanza kikao…kwa kasi hiyo hatuwezi kuendelea ni lazima tubadilike” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya alielezea masikitiko yake kwa kitendo cha madiwani na watumishi wengine kuendelea kuchelewa licha ya kufanya ziara ya mafunzo na kujionea Halmashauri nyingine zilivyopiga hatua kwa sababu ya kuzingatia muda.

Alisema kuwa ni vema Madiwani na Watumishi watambue kuwa muda ni uchumi na pia ni vema na watambue kuwa kila dakika wanayopoteza wajiletea hasara.

Naye Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo aliwaomba Madiwani wenzake kuufanyia kazi ushauri wa Mkuu huyo wa Wilaya kwa sababu utawasaidia kuongeza makusanyo na kuwa na fedha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa Manisapaa ya Tabora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad