HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 26 January 2018

AZAM FC WASEMA WATAIFUNGA YANGA KESHO

Na Agness Francis, Blog ya Jamii
MSEMAJI Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema licha ya Yanga wameshawahi kuutumia Uwanja wa Azam  Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam lakini wanaamini timu yao itaibuka na ushindi na kuchukua pointi tatu ambazo ni muhimu kwao na wamejiandaa vizuri.

Kauli ya Maganga inakuja kuelekea mtanange utakaopigwa kesho kwa kuzikutanisha timu hizo kesho saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.Azam FC ndio mwenyeji wa mchezo huo.

"Yanga wameshawahi kuutumia uwanja wetu  kwa ajili ya mechi zao za kirafiki lakini Azam FC ni mara ya kwanza kucheza na kikosi hicho katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,"amesema Maganga.

Akiwa katika Makao Makuu ya Azam, Maganga amesema "Tumejipanga  vizuri na tunaimani tutashinda kwa kunyakua pointi 3 dhidi ya mabingwa watetezi  Yanga,"amesema Maganga.

Kwa upande wa Nahodha wa Azam FC, Himid Mau amesema ushindi  kwao ni muhimu japokuwa kikosi cha Yanga kiko vizuri na ni timu kubwa hapa nchini na wanauwezo wa kucheza kabumbu la kiufundi zaidi.

Aidha Kocha Msaidizi AzamFc Iddy Cheche amesema kikosi chake kitaibuka na ushindi kwani maandalizi ni mazuri na wachezaji wako fiti kiakili na kiafya na wapo tayari kupambana kwenye mchezo huo.

"Tunaitaji ushindi wa pointi 3 ili kukaa kileleni  kumshusha Mnyama Simba,"amesema Cheche.
 Msemaji Mkuu Azam Fc, Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari  katika kuelekea mtanange wa kesho dhidi ya AzamFc na Mabingwa watetezi YangaSC, leo katika Makao makuu ya Azam Chamazi Jijini Dar es Salaam.
 Kocha Msaidizi Azam Fc, Iddy Cheche akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa kesho na wanamatumaini kuwa Ushindi ni wao.
 Nahonda wa kikosi cha AzamFc, Humid Mau Mkami akizungumzia jinsi walivyojipanga vizuri kukabiliana na mechi yao dhidi ya Yanga SC hapo kesho Katika makao makuu ya Azam Chamazi leo Jijini Dar es salaam.
 Beki wa kati wa AzamFc, Agray Mourris akizungumza  na waandishi wa habari kuwa wamejipanga vema dhidi ya mchezo wa kesho, katika makao makuu ya AzamChamazi Complex  leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad