HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 22 December 2017

YANGA YATEUA KAMATI YA MABADILIKO IKIONGOZWA NA ALEX MGONGOLWA


Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Klabu ya Yanga imeuanza rasmi mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa kumteua Wakili Alex Mgongolwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo..

Mgongolwa atasaidiwa na wajumbe watano ambao ni Mheshimiwa Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed Nyengi.

Kamati hiyo imetangazwa leo Ijumaa na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa ikiwa ni siku chache tu tangu watani wao Simba kupitisha mchakato huo na kumpata mwekezaji ambaye alishinda zabuni hiyo.

Yanga wao wamefuata Katiba yao ya mwaka 2010 inayoelekeza kuwa mwekezaji ni lazima awe na asilimia 49 na 51 ziwe za wanachama kwa maana ya klabu kama serikali ilivyofanya mabadiliko ya Katiba katika kipengele cha mfumo wa uendeshaji wa Hisa.

Mbali na hilo Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokukutana jana hii tarehe 21/12/2017 makao makuu ya klabu hiyo katika kikao maalumu,imeteua majina 28 ya wanachama kuunda kamati mpya ya mashindano.

Katika uteuzi huo,Hussein Nyika ameteuliwa kuwa mwenyekiti,Musatapha Ulungo,makamu mwenyekiti na Samuel Lukumay ameteuliwa kuwa katibu wa kamati hiyo.

Wajumbe wengine ni;
1.Omary Chuma
2.Hussein Ndama
3.Majid Suleiman
4.Mussa Katabaro
5.Yusuphed Mhandeni
6.Beda Tindwa
7.Jackson Maagi
8.Lameck Nyambaya
9.Nicko Meela
10.Edward Urio
11.Rogers Gumbo
12.Edigar Mutani
13.Shija Richard
14.Sanga Kayanda
15.Hamad Islam
16.Pascal Kihanga
17.Isiaka Sengo
18.Bahati Mwaseba
19.Rashid Msinde
20.Khalfani H.Kigwelembe
21.Yanga Makanga
22.Rogers Lamlembe
23.Leonald Chigango

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa Habari inaeleza kwamba majina ya wajumbe wengine wawili pamoja na matatu ya walezi na washauri wa kamati hiyo yatatangazwa baadae.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad