HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 22, 2017

RAIS WA TFF WALAACE KARIA KUKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI DEC 27 MWAKA HUU

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27, 2017.

Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.

Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.

Taarifa zaidi za mkutano huo wa Rais Karia na Wahariri,mahali utakapofanyika pamoja na mualiko utatolewa kwa vyombo vya habari.

Huu ni mkutano wa kwanza wa Rais Karia na Wahariri wa habari za Michezo tokea ameingia madarakani.

Rais Karia aliingia madarakani August 12, 2017 kwenye uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi ambao pia uliwaingiza madarakani Michael Wambura kwenye nafasi ya makamu wa Rais.

Wajumbe wa kamati ya utendaji waliongia madarakani kwenye uchaguzi huo ni pamoja na

Kanda namba 13 Dar es Salaam
Lameck Nyambaya

Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga
Khalid Abdallah

Kanda No 11 Pwani na Morogoro
Francis Ndulane

Kanda Namba 10 Dodoma na Singida 
Mohamed Aden

Kanda Namba 9 Lindi na Mtwara
Dunstan Mkundi

Kanda namba 8 Njombe na Ruvuma
James Mhagama

Kanda namba 7 Mbeya na Iringa
Elias Mwanjala

Kanda Namba 6 Katavi na Rukwa
Kenneth Pesambili

Kanda namba 5 Kigoma na Tabora
Issa Bukuku

Kanda namba 4 Arusha na Manyara
Sarah Chao

Kanda namba 3 Shinyanga, Simiyu
Mbasha Matutu

Kanda namba 2 Mara, Mwanza
Vedastus Lufano

Kanda namba 1 Kagera, Geita
Salum Chama

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF
Desemba 22,2017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad