HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2017

Washindi wa Promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde wakabidhiwa mkwanja wao

Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa Mary Rutta (aliyekaa kushoto) pamoja na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyekaa kulia) wakiwa pamoja na baadhi ya washindi wa zawadi za shilingi milioni moja na laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde'. Jumla ya wateja 55 wa Tigo wamejishindia donge nono katika promosehni hiyo inayoendelea ambapo wateja wa Tigo wanaofanya miamala kupitia Tigo Pesa wana fursa ya kujishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano. Pia kuna zawadi kubwa ya shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5 zinazoshindaniwa.
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza na baadhi ya washindi wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo wateja 11 wamejishindia zawadi za kila siku za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine 44 wakijishindia zawadi za kila siku za shilingi 500,000 kila mmoja. Pamoja na zawadi hizo za kila siku, zawadi kubwa katika promosheni hiyo inayoendelea ni shilingi milioni 15, milioni 10 na shilingi milioni 5.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad