HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 20, 2017

WAHAMIAJI HARAMU 55 WAMAKATWA WILAYANI MKINGA

ZAIDI ya wahamiaji 50 raia kutoka nchini Ethiopia wameka matwa eneo la Duga wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kiungia nchini kinyume cha sheria.

Wahamiaji hao wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Desemba mwaka huu kutokana na operesheni ambazo zimekuwa zikiendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ya kuhakikisha wanazibiti wimbi la uingiaji huo.


Hayo yalisemwa jana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga DCI, Crispian Ngonyani wakati akizungumza ofisi kwake ambapo alisema wahamiaji hao hivi sasa wanaendelea na kesi zao zinazowakabili kutokana na kuingia nchini kinyume na utaratibu uliopo.


Alisema hatua ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao inatokana na kuwepo kwa misako ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali hasa ya mipakani mkoani hapa ambapo wahamiaji hao wamekuwa wakitumia kama njia ya kuingilia.


“Sisi kama Uhamiaji mkoani Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha wimbi la wahamiaji haramu hawaingii kutokana na doria ambazo tumekuwa tukizifanya mara kwa mara lakini kubwa zaidi ni kuwepo kwa vituo eneo la mipakani hususani Horohoro “Alisema.


Aidha alisema pia ili kuhakikisha suala hilo linazibitiwa kwa vitendo tayari wamekwisha kuweka kituo eneo la Vijinga wilayani Mkinga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanakagua magari ambayo yamekuwa yakitokea nchini Jirani ya Kenya  ili kuweza kubaini iwapo wahamiaji haramu wamebebwa.


Hata hivyo alisema kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya wamejiandaa vizuri kuweza kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu wanaoweza kuingia mkoani hapa kwa kuendelea operesheni kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba za kulala wageni na kwenye hoteli.


“Licha ya kuendelea na operesheni hizo lakini nisema idadi ya wahamiaji haramu wanaoingia mkoani Tanga kwa sasa imepungua kwa sababu wakiwakamata wanawapeleka mahakamani pamoja na mawakala wao"Alisem

Afisa Uhamiaji huyo alisema lakini bado tunaendelea kuhakikisha ina koma kabisa kwa kuwachukulia hatua kali na watanzania ambao watabainika wanashirikiana nao kuwaingia mkoani hapa(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad