HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 18, 2017

VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA

Said Mwishehe, Blogu ya jamii
MWENYEKITI wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(TID) Profesa Apollinaria Pereka amewataka vijana  wasisite kuanzisha viwanda nchini  kupitia elimu ya ufundi waliyoipata kwenye taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa.

Pia  amesema  wasiogope changamoto watakazokumbana nazo na badala yake wawe wabunifu katika uanzishaji wa bidhaa zao.

Profesa Pereka amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mahafali ya 11 ya DIT ambapo amefafanua ,Serikali imejipanga kupiga vita umasikini, hivyo vijana ni vema wakaanzisha viwanda ili wajiajiri wenyewe.
Amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kulijenga taifa na kuanzisha viwanda endelevu.

Ameongeza nchi yenye maendeleo makubwa ni ile yenye ujuzi wa ufundi,na wanaotumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwanzishaji wa viwanda.
Pia amesema kwa sasa  DIT imefikisha miaka 60 tangu ianzishwe  na imefanya kazi kubwa kueneza elimu ya ufundi nchini.

“Utimizaji wa miaka 60 ya DIT imeenda sambasamba na serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha viwanda nchini kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi ,hivyo tutakwenda sambamba na serikali hiyo ili kutimiza azma ya Rais, Dk. John Magufuli,"amesema 

Awali Mkuu wa chuo hicho Profesa Preksedius Ndomba,amesema  Serikali ya awamu ya tano inalenga kuleta maendeleo ya viwanda vidogo,vya kati na vikubwa.

"Hivyo vijana wajiunge katika vyuo vya ufundi ili kuweza kupata ajira na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.

“Elimu ya ufundi ina umuhimu mkubwa katika serikali hii ya awamu yatano kwa sababu ya uwanzishaji wa viwanda nchini, vijana mjifundishe ufundi sanifu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe”amesisitiza  Profesa Ndomba.

Ameongeza DIT ipo sambasamba na Serikali katika kufanikisha  uanzishwaji wa viwanda, hivyo wapo makini katika utoaji wa elimu yao ili vijana wao wakimaliza wawe wasanifu wazuri katika viwanda vinavyokuja na kwamba wataendelea kupia watalaamu.
Mwenyekiti wa Baraza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), Prof.  Apollinaria Pereka akizungumza kwenye Mahafali ya 11 ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu  876 wamehitimu ngazi mbalimbali za kitaaluma za Stashahda, Shahada na Shahada za Uhandisi na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad