HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 18, 2017

WADAU WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSIADA WA KULINDA BINAFSI

Imeelezwa kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalifu unaohatarisha amani na kuongeza usalama wa mtu, jamii, nchi na dunia kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amesema hayo katika kikao cha wadau cha kupitia mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi na kusisitiza umuhimu wa kujielimisha kabla ya kusambaza taarifa.
“Ni muhimu kwa jamii kuelewa haki ya faragha ya mtumiaji wa mawasiliano na namna ya kushughulikia taarifa katika ukusanyaji, usambazaji, uchakataji na uhifadhi ili kuepuka kutenda uhalifu” amesema Dkt. Sasabo.
Dkt. Sasabo amezungumzia umuhimu wa jamii kuzingatia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 ili kuepuka makosa yasiyo yalazima na kuepuka usambazaji wa taarifa binafsi za watumiaji wa mawasiliano usiouwiana na maadili na wenye nia ovu.
“Ni vema jamii ikajua mitandao haina mipaka, hivyo ni muhimu kuwa na muongozo utakaosimamia haki za watumiaji na kulinda taarifa binafsi”, amesisitiza Dkt. Sasabo.
Naye, Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, amesema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamechangia ongezeko kubwa la makosa katika mawasiliano ya simu na intaneti hivyo uwepo wa sheria inayosimamia taarifa binafsi utapunguza changamoto za kimtandao na kuongeza haki ya faragha.
Dkt. Sasabo, alikuwa katika kikao kazi cha wadau kukusanya maoni ya mapendekezo ya kutungwa sheria ya kulinda taarifa za watumiaji ili kupunguza uhalifu na kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Usalama Mtandao, Eng. Stephen Wangwe.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma, leo.
 Wadau wa Sekta mbalimbali, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi,Mkoani Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wadau walioshiriki katika mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad