HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 4, 2017

UMOJA SWITCH YAHAMASISHA KUBADILI KADI

Umoja Switch inianzishwa miaka zaidi ya kumi iliyopita ili kuwezesha benki ndogo na za kati kuweza kupata huduma za ATM. Kupitia Umoja Switch benki zaidi ya 27 zinawezesha wateja wao kupata huduma kwenye ATM zaidi ya 250 bara na visiwani.Ili kuongeza usalama na pia kutua fursa ya kuongeza bidhaa zaidi, Umoja Switch ilianza mkakati wa kuhamisha wateja kutoka kwenye kadi za zamani zenye ufito (magnetic stripe) kwenda kwenye kadi mpya za kisasa na zenye usalama wa juu (Chip). Zoezi hili ambalo linaishia mwezi huu wa Disemba mwishoni.

Ili kuwazawadia wateja wake hususani wale wenye kadi zenye Chip, Umoja switch imeanzisha droo kubwa inayowezesha wateja kushinda fedha wanazotoa kwenye ATM maradufu,shilingi milioni moja,simu za mikononi au T-shirts za Umoja. Droo hii ni kwa wateja wenye kadi mpya ambao wanatumia ATM za Umoja popote Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Danfold Mbilinyi alisema “ Lengo kuu la umoja ni kusogeza huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi popote Tanzania. Tunafurahi kuwa tumeweza kufika maeneo mengi Nchini na bado tunalenga kuongeza kasi ya ubunifu na usogezaji wa huduma zetu. Kuboresha ubora wa kadi zetu ili kuongeza usalama na pia kutoa fursa zaidi ya ubunifu ni ishara tosha kuwa Umoja Switch inalenga kuwa msharika madhubuti wa Maendeleo ya Tanzania hususani sekta ya kifedha. Tunawakaribisha wateja wetu na hata ambao si wateja wetu kubadilish kadi au kufungua akaunti kwenye benki yeyote mshirika ili nao washinde kwenye droo hii kubwa“.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad