HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 6 December 2017

TIB CORPORATE BENKI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MATIBABU KWA ZAHANATI YA MSONGOLA- ILALA

Benki ya TIB imetoa msaada wa vitanda viwili pamoja na mashine ya kupumulia kwa mtoto mwenye tatizo la kupumua katika zahanati ya Msongola , Ilala jijini Dar es Dar es Salaam.
Akizungumza baada kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo amesema kuwa benki inaguswa na afya za wananchi pamoja na watoto.
Amesema kuwa benki itaendelea kutoa msaada mbalimbali kwa ajili ya wananchi wake ambao ndio mtaji wa benki pale wanapopata huduma bora za afya.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema msaada huo ni muhumu katika zahanati ya Msongola na kuwata benki hiyo kuendelea kuunga mkono zahanti katika kuweza kutoa huduma bora.
Amesema serikali ina mambo mengi pale panapotokea wadau wanajitolea wanakuwa wameisaidia serikali katika kutatua changamoto  na kuweza kuendelea kutoa huduma nyingine sehemu zenye changamoto.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo(kulia) akimkabidhi vifaa vya matibabu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema  kwa niaba ya Zahanati ya Msongola vyenye thamani ya shilingi milioni saba (7) walizochanga wafanyakazi wa benki hiyo ili kusaidia wakina mama wanaojifungua katika Zahanati hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Ukonga,  Mwita Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari, wafanyakazi wa TIB Corporate Benki, Wauguzi na wananchi wa Msongola mara baada ya TIB Corporate Benki kukabidihi msaada wa vifaa vya matibabu kwenye Zahanati ya Msongola leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu benki hiyo inavyorudisha fadhila kwa wananchi kwa kusaidia kwenye masuala ya kijamii ikiwemo na msaada walioutoa kwenye Zahanati ya Msongola.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Msongola,  Dk. Mwanahawa Malika akitoa shukrani kwa TIB Corporate Benki kwa kusaidia zahanati hiyo 
Baadhi vifaa vilivyotolewa na TIB Corporate Benki kwenye Zahanati ya Msongola leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa TIB Corporate Benki wakiwa kwenye picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad