HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 14, 2017

TIA yahamasisha wahadhiri kuandaa tafiti na machapisho


Na Said Mwishehe wa Globu ya Jamii
TAASISI ya Uhasibu Tanzania(TIA) imesema kuwa kuna umuhimu wa wahadhiri  kufanya tafiti na machapisho mbalimbali kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wao.

Kufanya utafiti huo na kuweka katika machapisho yatasaidia walimu kutoa taaluma ya uhasibu na biashara inayokwenda na wakati.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dk.Joseph Kahanda wakati anaelezea mikakati yao ni  kuandaa na kuwajenga  wahadhiri kitaaluma  katika kuwaanda wahitimu katika soko la ajira.

“Tumeamua kufanya kongamano ambalo lengo lake ni kujadiliana na walimu wetu na hasa kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti na machapisho kwa ajili ya kusaidia  katika majukumu yao ya kupima wataalamu kwenye fani zinazotolewa chuoni kwetu.

“Walimu wasipofanya tafiti na kutoa machapisho kuna uwezekano wa kuendelea kutumia tafiti na machapisho yaliyopitwa na wakati.

“Hivyo tunahimiza walimu wetu kufanya tafiti zitakwenda na wakati na kutowaacha nyuma kitaaluma wanaowafundisha,”amesema Dk.Kihanda.

 Pia amesema wanafunzi wanasoma kwenye taasisi hiyo wamekuwa na soko kubwa la ajira pindi wanapohitimu.

Amesema kuwa kuna mashirika na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikiomba wanafunzi wanapohitimu kuwapatia ajira na hivyo kimefanya kuwa kimbilio la wengi.

Kuhusu mahafali ya 15 ya taasisi hiyo yanayofanyika leo, amesema kwa  Dar es Salaam  wahitimu 3,833 wanatunikiwa vyeti.

Amefafanua mahafali mengine ya taasisi hiyo yatafanyika pia katika tawi lao la mkoani Mtwara.Hivyo jumla ya wahitimu wote wa Dar es Salaam na Mbeya ni zaidi ya 5,840.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad