HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 6, 2017

SERIKALI YATAKA UMILIKI WA HATI MOJA YA UMILIKI WA UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kuweka utaratibu kwa wamiliki wa viwanja ndani ya uwanja wa ndege kuondoa ili kuwa na hati moja ya uwanja kwa kumilikiwa na mamlaka hiyo.

Hayo aliyasema leo Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye wakati alipotembelea uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni mbili ambazo zina hati katika uwanja wa ndege ni Tanzanair pamoja na Puma Energy ambazo zilipata ardhi kwa taratibu.

Amesema Mamlaka ndiyo ndiye ina mamlaka ya kuwa na hati ya ardhi pasipokuwepo kwa kampuni kuwa hati ya umiliki ndani ya uwanja wa ndege.

Mhandisi Nditiye amesema nyumba  59 ambazo ziko katika uwanja wa ndege na zimekubali mamlaka ifanye utaratibu wa kutwaa eneo hilo.

Aidha ametaka TAA kuwa karibu kwa moja kwa moja na puma energy wakati wanachukua mafuta pamoja kuweka katika ndege ili serikali iweze kupata mgawo wake vizuri na sio kuendelea kuchukua takwimu.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard Mayongela amesema kuwa suala la umiliki wa hati watafatilia katika wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Amesema mameneja wote nchini wa uwanja wa ndege kuweka alama za mipaka na atakayeshindwa kufanya hivyo bora akapisha ili kuweza kuondokana na migogoro ya ardhi na wananchi.
 Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye akizungumza na Menejimenti ya viwanja wa ndege nchini (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard Mayongela akizungumza juu ya utekelezaji wa maagizo ya Naibu wa Waziri wakati alipotembelea uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta  Nditiye akipata maelezo kuwa Naibu Meneja wa Ghala la Mafuta la Puma Energy katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela  katika ghala la mafuta la Puma Energy wakati Naibu waziri alipofanya ziara katika uwanja wa mwalimu Julius Nyerere.
Sehemu kalakana ya Tanzanair katika uwanja wa ndege wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad