HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 14 December 2017

SERIKALI IMETUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 500 KUKAMILISHA MRADI MKUBWA WA UMEME WA KV 400 KUTOKA IRINGA HADI SHINYANGA

Na Jumbe Ismailly 
SERIKALI imetumia zaidi ya shilingi bilioni 500 kugharamia mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme wa msongo wa KV 400 ulioanza kutekelezwa mwaka 2016 na kukamilika mwaka 2016  kutoka Mkoani Iringa kupitia Dodoma, Singida, Tabora hadi mkoani Shinyaga.

Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula alisema kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotumika kusambaza miundombinu hiyo ya nishati ya umeme, haina budi kuhakikisha inalindwa na kila mwananchi na inakuwa salama kwa wakati wote ili huduma hiyo iweze kuendelea kupatikana.

Aidha meneja huyo aliweka bayana kwamba kwa hiyo inapotokea mhalifu mmoja anapokwenda kuchukua na kuangusha nguzo ulipopita umeme huo wa msongo wa taifa na kuanguka chini, serikali huingia hasara kubwa sana na kwamba idadi kubwa ya wananchi hukosa huduma hiyo ya umeme.

Kwa mujibu wa Kaihula gridi ya taifa imeungana na kwa hali hiyo endapo njia moja itaanguka na kuchangia kukosekana kwa umeme, itasababisha pia mikoa yote iliyoungamishwa katika gridi ya taiafa kukosa pia huduma hiyo ya umeme pia.
Meneja huyo wa njia kuu za umeme aliyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iramba pamoja na Kijiji cha Misigiri alipokuwa akitoa ufafanuzi wa ziara ya watendaji wa TANESCO katika wilaya hiyo ikiwa ni sambamba na kutoa elimu kwa wananchi wa eneo hilo juu ya kukabiliana na matukio ya wizi na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika njia kuu ya msongo wa taifa wa KV 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga.
“Sasa mikoa ikikosa umeme ina maana nchi inakuwa katika hali ambaayo siyo ya usalama na kutakuwa na athari kubwa kijamii kutokana na hospitali zetu zinategemea umeme na hata uchumi wa kila mmoja wetu utaanguka kwa kuwa uzalishaji pia utapungua kwa kukosa nishati hiyo ya umeme” alifafanua Meneja huyo wa njia kuu ya umeme.

Kwa upande wake Afisa usalama TANESCO Mkoa wa Singida,John Chilale amepiga marufuku biashara ya kununua miundombinu chakavu ya Tanesco pamoja na wanaokwenda kuuza miundombinu hiyo kwa sababu  pia ni kosa la jinai na la uhujumu uchumi.

“Kwa hiyo wanaonunua vyuma chakavu waache kununua miundombinu inayotokana na miundombinu ya Tanesco na wanaoend kuuza vilevile ni hatari kwa sababu ni kosa la jinai”alisisitiza afisa usalama huyo wa Tanesco Mkoa wa Singida.

Hata hivyo Chilale alibainisha pia kwamba kuna watu wanaojaribu kupanda kwenye nguzo hizo na kufanya shughuli kwamba ni hatari na kuwatahadharisha wananchi hao kutofanya shughuli zozote karibu na nguzo hizo na hivyo kuwataka kujiepusha kabisa na vitendo hivyo.

“Kwa hiyo wanaonunua vyuma chakavu waache kununua miundombinu inayotokana na miundombinu ya Tanesco na wanaoenda kuuza vile vile ni hatari kwa sababu ni kosa la jinai”alisisitiza afisa usalama huyo wa Tanesco Mkoa wa Singida.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iramba,Emmanueli Luhahula aliwatahadharisha watu wote wanaotarajia na wanaoashiria kujihusisha na vitendo vya kuhujumu miundombinu ya Shirika hilo la Tanesco kuwa waache mara moja na endapo watajihusisha serikali haitawafumbia macho.

Hata hivyo Luhahula ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba pamoja na kulishukuru shirika la ugavi umeme (Tanesco) kwa ushirikiano wake inaotoa kwa uongozi wa wilaya hiyo,lakini vile vile hakusita kutoa wito kwa wananchi wilayani hapa kwamba wawe walinzi wakubwa wa miundombinu ya shirika hilo.

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Emmanueli Luhahula akitoa maelezo ya jitihada zinazofanywa na wilaya hiyo kwa kushirikiana na TANESCO kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika wilaya hiyo.
 Afisa usalama wa TANESCO Mkoa wa Singida,John Chilali (wa kwanza kutoka kushoto) akibadilishana mawazo nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iramba na afisa mahusiano wa shirika hilo Mkoani Singida, Witness Msumba (wa pili kutoka kushoto). 
 Meneja Njia kuu za umeme, Amosi Kaihula akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya fedha zilizotumika kukamilisha mradi huo mkubwa wa KV400 na mikakati ya kukabiliana na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika njia kuu ya kusambazia nishati hiyo.
Nyaya za kusambazia umeme katika njia kuu ya kutoka Mkoa wa Iringa hadi Shinyanga yenye msongo wa KV400(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad