HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 12, 2017

ONE STOP CENTRE YAWATAKA WADAU KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WATOTO

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Edina Sanga (wa pili kushoto) akiwa na Afisa Polisi Kutoka dawati la Jinsia Christina Onyango na wadau mbalimbali wa masuala ya ukatili wa kijinsia.
 
Katika kusaidia kupinga ukatili wa kijinsia, kituo cha usuluhishi( Crisis Resolving Centre- CRC) kimejizatiti katika kutetea haki za binadamu kwa kulinda haki na ustawi wa watoto na wanawake.

Kituo hicho kilichoanzishwa 2007 kikiwa na mlengo wa utoaji huduma ya msaada wa kisheria  na ushauri nasaha kwa jamii.

Akizungumzia kazi zinazofanywa na CRC, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi CRC Gladness Munuo amesema kuwa mnano Novemba 14 hafi 16 kimeweza kutoa ya huduma ya pamoja  kwa wahanga wa wa ukatili wa kijinsia  ijulikanayo kama One Stop Centre ikiwa inawalenga wakina mama na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa ukatili wa kijinsia.
Gladness amesema katika huduma ya pamoja na One Stop Centre  waliweza kutoa huduma kwa wateja 25 waliotembelea  kituo kwa kuhitaji msaada wakisheria na ushauri nasaha  ambapo wanawake walikuwa 22, wanaume 2 na mtoto mmoja.

Katika kesi hizo kesi mbili ziliweza kuhamishwa kutoka kituoni ambazo ni mgogoro wa ardhi na nyingine ilihusu kesi ya mauaji ambapo iliwezw kuhamishiwa polisi.

Ameelezea kuwa, katika usulihishi wa kifamilia uliweza kufanyika kwa wateja wanne na mashauri mawili ndio yaliyofanikiwa na nyingine ilikuwa ni matunzo ya mtoto.

Huduma ya one stop centre inajumuisha utolewaji wa huduma za pamoja kwa wakati mmoja, huduma hizo ikiwemo msaaxa wa kisheria na ushauri nasaha kwa wakati mmoja. Ambapo taasisi nyingi za msaada wa kisheria zimekuwa zikijihusisha na msaada wa kisheria pekee bila ya kuhusisha huduma nyingine shiriki ambazo ni muhimu kufikia hitimisho zuri la tatizo la mteja.

Kituo cha Usuluhishi (CRC) kiliona umuhimu wa kutumia one stop centre model kwa kuanzisha utaratibu wa kila mteja atanufaika na huduma ya ushauri nasaha kutoka kwa wanasheria sambamba na afisa ustawi wa jamii.

One stop centre ni sehemu yaa hospital ambapo hutoa huduma mbalimbali kama madawa, saikolojia, msaada wa kisheria na ulinzi kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia (GBV na VAC)

Malengo makuu ya kuanzishwa kwa one stop centre kwa ushirikiano na wadau wengune kama polisi dawati la jinsia, madaktari, afisa ustawi wa jamii na wasaidizi wa kisheria ni kutoa huduma za kutosha kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia kwa wakati sahihi pindi anapofika katika kituo cha afya.

Muathirika wa ukatili wa kijinsia akishafika katika kituo cha one stop centre anaweza kupata msaada zaidi kwa kupewa rufaa ya kwenda kupata huduma maalumu za kisheria , saikolojia na ustawi wa jamii.

Christina Onyango ni afisa wa polisi ila ni msimamizi wa kituo cha One stop Centre katika hospitali ya Amana ameelezea hatua mbalimbali wanazozifanya pindi wanapopokea muathirika wa ukatili wa kijinsia mpaka kupata huduma pamoja na matibabu pindi inapohitajika.

Christina amesema, jamii haitakiwi kufumbia macho masuala ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kwani ndio waathirika wakubwa  na wengi wanaofika kupatiwa huduma wanakuwa wamefanyiwa na watu wao wa karibu.

Ameweka wazi kuwa, kuna kesi zingine zinahusu masuala ya familia inapelekea kumchukua muathirika wa ukatili wa kijinsia na kuamua kumpeleka kwenye Nyumba ya Amani kwa ajili ya kukaa na kupatiwa huduma.

Ametoa rai kwa waandishi wa habari kuwa wavumilivu  pindi wanapotaka kuripoti na kupata taarifa za matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kwani kuna muda utakapoamua kuweka wazi kwa wananchi unaweza kusababisha kumuweka hatarini muathirika mwenyewe na kupoteza ushahidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad