HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 25 December 2017

NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI

Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa kuitupa rufaa iliyowasilishwa na mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha AFP.

Mgombe huyo alikuwa akipinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea  mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Mkurugenzi  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ramadhan Kailima amesema leo jijini Dar es Salaam kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kailima kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, NEC ilipokea rufaa moja kutoka kwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Pia NEC ilipokea rufaa mbili, ya kwanza iliwasilishwa na mgombea wa udiwani Kata Keza – Halmashauri ya Wilaya Ngara kwa tiketi ya CCM akipinga uamuzi wa Msimamizi  wa uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea mgombea wa NCCR - Mageuzi.

Wakati rufaa ya pili ilitoka kwa mgombea wa udiwani Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya Korogwe kwa tiketi ya CCM akipinga aumuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomuwekea mgombea wa Chama cha Wananchi(CUF.

Kailima amefafanua kwenye kikao chake cha kawaida kilichofanyika Desemba 24, mwaka huu, NEC ilipitia rufaa hizo na kutoa uamuzi.

Akizungumzia rufaa ya mgombea ubunge,NEC  imekubaliana na uamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi,hivyo  mgombea aliyekatiwa rufaa aendelee kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Amesema kuhsu rufaa za wagombea udiwani kata ya Keza na  Kwagunda, NEC imekubaliana na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi.

“Hivyo wagombea udiwani waliokatiwa rufaa waendelee kuwa wagombea wa udiwani katika kata husika,”amsema Kailima.

Ametumia nafasi hiyo kueleza tayari NEC imetuma taarifa ya uamuzi huo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili watoe taarifa kwa wahusika kuhusu kilichoamriwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad