HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 27 December 2017

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AZINDUA UMEME WA REA KATA YA MWASENI WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu amezindua mradi wa umeme wa vijijini REA awamu ya pili katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni Rufiji  Mkoa wa Pwani sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Naibu Waziri aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ambapo kwa pamoja waliweza kuzungumza na wananchi hao wakizidi kuwasisitiza kujiunganisha na mradi wa umeme wa REA kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi kwa nishati hiyo muhimu.

Kabla ya kuzinduliwa kwa umeme huo, Naibu Waziri wa Nishati Subira aliweza kupewa taarifa rasmi ya toka kuanza kwa mradi huo wa umeme vijijini REA kutoka kwa Meneja wa TANESCO kutoka Wilaya ya Rufiji Basilus Kayombo ambapo alisema kuwa mradi huo rasmi kwa kijiji cha Mloka ulianza mwaka 2014, na ujenzi wake kuanza 2015 na kumalizika Novemba 2017 na kugharimu takribani bilion 2.5 za kitanzania kutoka Ikwiriri mpaka kufika Mloka.

Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua meadi wa umeme wa vijijini REA, Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira, alisema kuwa nia kubwa ya serikali kuleta huduma ya nishati karibu na wananchi ni katika kuchagiza maendeleo yakiwemo wananchi kwa pamoja kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.

Subira amesema kuwa, Mbali na hilo serikali ya awamu ya Tano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wameweza kudhamiria na kuanza harakati za ujenzi wa bwawa la Rufiji Stigilas litakalotoa megawat 2100 na kuingia katika gridi ya taifa ambapo bwawa hilo litakuwa katika kata ya Mwaseni na itawanufaisha wananchi wa eneo hilo kujipatia ajira pale ujenzi utakapoanza pia watafaidika na mradi huo.

Naibu Waziri amewaagiza TANESCO kuendelea kuunganisha umeme kwa wananchi kwani Wizara bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na kusitisha kwa uunganishaji wa umeme huo ambao ni nafuu hususani kwa wananchi wa vijijini pia gharama yake haijabadilika bali bado ni ile ile 27,000 kwa kila kaya.

Mbali na uzinduzi wa Umeme huo, Subira amewataka wananchi wa kata na vijiji mbalimbali kujitoa zaidi katika kuleta maendelo ya vijiji vyao ikiwemo kwenye kuchangua ujenzi wa zahanati kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanapokwenda kujifungua na hata wao wenyewe pindi wanapokuwa wanaumwa.

Katika kituo cha Afya cha Mwaseni na Nyaminywili Naibu Waziri aliweza kuchangia mifuko 50 ya sarufi kwa kila kimoja huku mdau mwingine wa maendeleo alitoa mifuko 100 katika zahanati ya Nyaminywili na mabati 100 pamoja na mifuko ya saruji 30 kwa zahanati ya Mkongo kwa ajili ya kumalizia jengo la wodi ya wakina mama na wazazi.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali kabla ya kuanza ziara yake ya siku mbili katika Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa umeme wa REA kwenye Kata ya Mwaseni Rufiji Mkoa wa Pwani.
 Mhandisi wa Umeme kutoka Mkoa wa Pwani Eng. Seleman Mghwira akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu kabla ya kuanza kwa ziara.
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo akizungumza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya siku mbili katika Wilaya hiyo ya Rufiji.
 Meneja wa TANESCO Wilaya ya Rufiji, Sabilus Kayombo akielezea mradi wa umeme wa vijijini REA katika kata ya Mwasene wenye takribai Kilomita 100 kutoka Ikwiriri ulivyoanza mpaka kufikia tamati Novemba mwaka huu na kugharimu takribani bilioni 2.5 ulioanza kujengwa 2015.
 Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji na kujionea maendeleo ya mradi wa umeme vijijini REA ulipofikia na kuwataka wananchi waendelee kujiunganisha kwa kujaza fomu ili kuweza kupata umeme kwa ajili ya kuchagiza maendeleo ya kiuchumi ndani ya mkoa wa Pwani. 
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua baadhi Zahanati wakati wa ziara yake ya siku mbili ndani ya Wilaya ya Rufiji.
 Wananchi wa kijiji cha Kipo kata ya Kipugila wakionesha malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ya kushindwa kupata umeme wa REA ingawa miundo mbinu ikiwemo nguzo za umeme zimepita katika maeneo yao Kijijini hapo na Naibu Waziri kuwaagiza TANESCO kuweza kuhakikisha kabla hawajaenda kata nyingine wahakikishe vijiji vyote vinne vinapata umeme huo.
Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu akikagua kisima cha maji cha Kata ya Mkongo kinachoendesha kwa nguvu ya rasilimali ga mafuta kutokana na kutokuwa na nishati ya umeme kwenye eneo hilo na kupelekea wananhi kununua maji kwa bei kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad