HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 28 December 2017

MWILI WA MAREHEMU MAYAGE WAAGWA LEO NYUMBANI KWAKE MBWENI


Na Said Mwishehe, Blogu  ya Jamii
TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonyesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi.

Hayo yamesemwa leo  mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es  Salaam.

Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua akipata kitandani Manage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.

Alisema msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.

Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage  S. Mayage katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi na alichojifunza ni upendo na uvumilivu. 

"Alikuwa ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa zaidi ni kumuombea kwa  Mungu, "amesema Padre Kaniki. 
  
Mayage S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani  na  nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.

Ilipofika mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia Tanzania. 

Akizungumza katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika taaluma. 

Kibanda amesema mchango wa Mayage katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa.

"Mimi na Mayage pamoja na wengine tuliojariwa pamoja Habari Coparation, anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu kitaalum.

MWILI WAWASILI NYUMBANI KWAKE
Mwili uliwasili saa saba na nusu ambapo maombi yalianza kama ratiba ilivyoeleza huku waombolezaji wakiendelea kuwasili.

Miongoni mwa wanahabari waliofika ni wahariri wa vyombo mbalimbali vya magazeti na luninga wakiongozwa na Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba.

Wengine ni wanasiasa ambapo waziri wa zamani wa Habari, Nape Nauye aliwasili akifuatiwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole. 

Marehemu ni miongoni mwa wanahabari waliozunguka katika vyumba vingi vya habari, hali hiyo imefanya kuwepo kwa wanahabari wengi msibani.
Padre wa Kanisa Katoliki, John Kaniki akiongoza misa ya kuombea mwili wa marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafamilia wa marehemu, ndugu na jamaa wakiwa fuatilia ibada ya kuagwa kwa aliyekuwa mwandishi mkongwe Mayage S. Mayage nyumbani kwake Mbweni Kijijini leo.
 Neno la Mungu likisomwa 

Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari, Nape Nauye na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole pamoja na ndugu na jamaa wakiwa kwenye ibada ya mazishi Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibada ya kuagwa kwa mwili wa Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad