HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 28 December 2017

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameagiza mkandarasi wa mradi wa umeme wa Vijijini REA awamu ya pili Kwa Mkoa wa Pwani ambayo ni kampuni ya MBH kuchukuliwa hatua hatua kali za kisheria.

Hatua hiyo imefikia baada ya mkandarasi huyo Kampuni ya MBH kushindwa kutimiza malengo ya mkataba na kuacha baadhi ya maeneo yakiwa hajaweka miundo mbinu ya umeme kama walivyokubaliana awali.

Akitoa maagizo hayo mbele ya wananchi wa Kata ya Ruauke, Naibu Waziri Nishati Subira amewataka REA kuhakikisha suala la mkandarasi huyo linachukuliwa hatua kwani ameweza kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakamilika na tayari mkataba wake ukiwa umeshamalizika.

Subira amesema maeneo mbalimbali ya ikiwemo Mkamba, Kisarawe, Kibaha Vijijini, Mkuranga, Kibiti, Kisiju na hata Rufiji kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakilimika na mengine akiacha nguzo za umeme zikiwa zimesimama bila kuwekwa nyaya za umeme.

"REA lazima muhakikishe mkandarasi huyu anachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kushindwa kufikia malengo kwani kuna maeneo mengi ameshindwa kutimiza malengi tuliyokubaliana na tayari mda wake ukiwa umeisha tayari wa kuweka miundi mbinu ya umeme,'amesema Subira.

Naibu Waziri amesema kuwa  Kwakuwa amehakikishiwa vifaa vya maeneo hayo bado vipo basi watazungumza na TANESCO au REA na kuangalia ni namna gani waje kumalizia na kuweka nyaja ili umeme uanze kuwaka katika kata ya Ruauke.

Mbunge wa Jimbo La Kibiti Seif Ally Ungando akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati waliweza kutembelea shule ya Sekondari Mtanga Delta iliyopo katika kijiji cha Uruma na kujionea changamoto ya Nishati ya umeme inavyochelewesha maendeleo kwenye eneo hilo.

Mbunge Ungando amemuomba Naibu Waziri Nishati kuwasaidia wananchi wa eneo hilo kupata umeme kwani wamekuwa na kiu hiyo kwa muda mrefu kwani hata hiyo shule ya Sekondari Mtanga Delta inayoweza kuhudumia wanafunzi kutoka vijiji vinne wamekuwa wanasoma kwa shida kutokana na kukosekana kwa nishati hiyo ya umeme.

Meneja Mradi wa REA Mkoa wa Pwani Mohamed Sauko ameweza kusema kuwa katika kijiji cha Ruauke,Kikale, Mchukwi,Nyamatanga mkandarasi aliweza kuingia katika mvutano na wananchi baada ya kuanza kukata mali za wananchi hao bila kuanza makubaliano na kupelekea mradi kuishia kuwekwa Nguzo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri aliweza kuchangia kiasi cha laki 2 kila mmoja kwa jukwaa la wanawake wa kijiji cha Ruauke  na Mchukwi kwa ajili ya kujiendeleza kimaendeleo pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa muendelezo zahanati  ya Nyamatanga.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika shule ua sekondari ya Mtanga Delta na kujionea maendeleo ya shule hiyo ikiwemo changamoto ya nishati ya umeme na kuwaahidi kulifanyia kazi kwa juhudi zake hasa baada ya Wizara ya Elimu kuipatia kiasi cha shiling Milion 256 kwa ajili ya kuendeleza miundo mbinu, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Shaban Kiffu.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua miundo mbinu ya shule ya Mtanga Delta akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kibiti Shaban Kiffu,Mbunge wa Jimbo la Kibiti Seif Ally Ungando, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoye na Mkuu wa Shule ya Sekondari hiyo Humphrey Mwakyambiki.
  Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Shaban Kiffu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uruma kichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Uruma kilichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara yake ya katika Wilaya ya Kibiti.
Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu akiwa kwenye picha ya pamoja na jukwaa la wanawake la Ruauke baada ya kumkabidhi zawadi ya mkeka.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wakina mama waliokuwa wamewapeleka watoto wao kupata chanjo katika kituo cha afya kilichopo Kijiji cha Muyuyu wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikabidhi mifuko ya saruji 50 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Seif Ally Ungando kwa diwani wa kata ya Ruauke, Mwarami Mkopi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Nyamatanga wakati wa ziara yake ndani ya wilaya ya Kibiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad