HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 12, 2017

KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA.

Na WAMJW - Dodoma 
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania  Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani  unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali 
Kamanda Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote  ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi  wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili  na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike  na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri na 
Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati  na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda  miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 ilikua 639, vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376, vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye  Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia  Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo  zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni  vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.
 Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani  Bi. Marlin Komba  anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.
 Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Baadhi  ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu hayupo pichani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad