HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 21 December 2017

JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI

Wanafunzi watano wa shule za Msingi za serikali hapa nchini wameshinda shindano la uchoraji la “Ishi Huru” ambalo liliandaliwa na Kampuni ya The Jubilee Insurance Company of Tanzania Limited na Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited. Walioshinda wamepewa zawadi za bima za Elimu za jubilee Life insurance, yaani “Jubilee Career Life Cover” watakayoipata watakapoingia elimu ya sekondari.

Shindano hilo liliendeshwa nchi nzima kwa kupitia TAMISEMI ambapo wanafunzi watano wameibuka kidedea baada ya kuchora na kutuma picha hizo.

Director of Surveillance and prudential supervision wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Mr. Elia Kajiba ameishukuru Jubilee Insurance kwa kuendesha shindano hilo ambalo limeweza kuwapa zawadi wanafunzi watano ya kuwa na uhakika wa kugaramiwa katika elimu yao ya sekondari.

Amesema kuwa waendelee kuandaa mashindano na vitu mbalimbali ambavyo vitainufaisha jamii na kuwasukuma wanafunzi kushiriki.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited ambaye pia ni Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya The Jubilee Insurance Company of Tanzania Limited, Mr. Shabir Abji amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Jubilee Insurance , uongozi wa kampuni hiyo iliamua kuishirikisha jamii katika kusheherekea na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii kama zawadi hizi kwa wanafunzi walioshinda shindano la uchoraji, kujenga na kuboresha vyoo vya shule za msingi nane hapa nchini, kujenga nyumba za walimu na madarasa ya shule kadhaa hapa nchini.

Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya amesema kuwa, anayo furaha kubwa sana kwani mtoto wake amemuwezesha yeyekufika Dar es Salaam na kupokea zawadi ambayo itamuhakikishia elimu yake ya Sekondari kutoka Jubilee Insurance.

Amesema kuwa Jubilee Insurance imekuwa ya kwanza kuwafikia wananchi wa kawaida kwa kutafuta vipaji vya wanafunzi.
Mwenyekiti wa bodi ya Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited ambaye pia ni Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya The Jubilee Insurance Company of Tanzania Limited, Mr. Shabir Abji , akizungumza na wageni waalikwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda kwenye shindano la uchoraji la “ Ishi Huru” la Kampuni ya Jubilee Insurance lililofanyika hapa nchini.
Mgeni rasmi Director of Surveillance and prudential supervision wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Mr. Elia Kajiba akitoa shukrani kwa Kampuni ya Jubilee Insurance kwa kuihudumia jamii pamoja na kuwasisitiza waendelee kujikita hasa kwenye kaya zenye kipato cha chini ili kuinua jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited, Helena Mzena akitoa historia ya shindano lililoshirikisha shule za msingi hapa nchini kwa wanafunzi wa darasa la Tatu , katika sherehe za ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi watano walioshinda. 
Chief Executive Officer wa kampuni ya The Jubilee Insurance Company of Tanzania, Mr. Dipankar Acharya akizungumza ujumbe mfupi katika sherehe zautoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi waliofanya vizuri kwenye shindano la uchoraji la “Ishi Huru”.
Mgeni rasmi Director of Surveillance and prudential supervision wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Mr. Elia Kajiba akimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa shule ya msingi Msasa, Khadija Mohamed Ali aliyeshinda kwenye shindano la uchoraji lililoandaliwa na Kampuni ya Jubilee Insurance.
General Manager wa kampuni ya Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited, Mr. Kumar Sumit Gaurav (kushoto) akimkabidi zawadi Mwanafunzi wa Shule ya msingi Katete, Atupele Wiston wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye shindano la uchoraji lililoandaliwa na Kampuni hizo mbili za Jubilee Insurance hapa nchini.
Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya akitoa shukrani kwa kampuni ya Jubilee Insurance kwa kujikita zaidi kwenye jamii pamoja na kumfadhili mtoto wake kupata bima ya Elimu ya Jubilee Life Insurance ambayo itamsaidia atakapofika elimu ya Sekondari.
Wanafunzi watano walioshinda, wazazi wao, pamoja na wafanyakazi wa Jubilee Insurance wakifuatilia mada wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye uchoraji wa shindano la “Ishi Huru” la Jubilee Insurance.
  
Mwalimu wa Shule ya Msingi Msasa, Josephine John Majili akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari waliofika kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi waliofanya vizuri kwenye shindano la uchoraji wa picha za shindano lililoandaliwa na Kampuni ya Jubilee Insurance.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad