HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 12, 2017

DK MGALULA ASHAURI WATANZANIA KUWA NA UZALENDO KWA NCHI YAO

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza vifaa Tiba cha Msagara, Dk.Ibrahim Mgalula akizungumza na Michuzi TV kuhusu jitihaza wanazofanya kutafuta ufumbuzi wa changamoto za uhaba wa vifaa tiba nchini huku akionesha baadhi ya aina za bidhaa wanazozalishwa kiwandani hapo kilichopo Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe wa Blogu ya Jamii
WATANZANIA wameshauriwa kuwa na uzalendo wa nchi yao kwa kutafuta suluhu ya ufumbuzi wa changamoto zilizopo nchini huku wakihimizwa pia kuunga mkono jitihada za Rais Rais, Dk. John Magufuli katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza vifaa Tiba cha Msagara kilichopo Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam Dk.Ibrahim Mgalula wakati akielezea jitihaza za kiwanda chake kusaidia kutafuta ufumbuzi wa changamoto za uhaba wa vifaa tiba.

Amesema kuwa kitaaluma yeye ni daktari wa magonjwa ya binadamu lakini aliamua kutumia nafasi yake kufanya utafiti maeneo mbalimbali nchini hasa ya upatikanaji wa vifaa tiba na kubaini kuna tatizo la ukosefu wa vifaa hivyo, hivyo katika kutafuta ufumbuzi wake waliamua kuanzisha kiwanda hicho.

Dk. Mgalula amesema anatambua mchango wa viwanda vya ndani katika kuimarisha uchumi wa nchini  hivyo wamedhamiria kuunga mkono juhudi za Rais katika sekta ya viwanda kwani mpango wao ni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba Bagamoyo, mkoani Pwani.

"Nchi zote ambazo zimepiga hatua katika mambo mbalimbali zimefika hapo kwasababu tu ya kutanguliza uzalendo kwa nchi yao. Badala ya kuuliza nchi imefanya nini kwa ajili ya wananchi wake , ni wakati wa sisi wananchi kujiuliza tumeifanyia nini nchi yetu,"anasema.

Kuhusu vifaa tiba ambavyo wanadhalisha kwenye kwanda chao anasema wanafarajika kuona Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto na Serikali kwa ujumla kutambua uwepo wao na vifaa tiba na hasa magozi yanayotumika kwenye huduma za upasuaji.

Amesema vifaa vita ambavyo vinatengenezwa kwenye kampuni yao lengo lake zaidi ni kumsaidia Mtanzania ambaye anatumia gharama kubwa katika huduma za afya, hivyo wao wameamua kuuza vifaa tiba kwa gharama nafuu zaidi lakini katika ubora wa hali ya juu ambao umethibitisha Shirika la Viwango Tanzania(TBS) na Shirika la Afya Duniani(HWO).

Kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli, Dk. Mgalula amesema kuwa Rais anafanya kazi wakati anaanza hakuwa anamuelewa lakini sasa  ameanza kumuelewa na anamuunga mkono kwa asilimia 100 na kuomba Watanzania wote nao kumuunga mkono ili afanikishe malengo yake ya kulitumikia Taifa.

Ametoa ombi kwa Serikali kuisaidia kiwanda hicho katika kufikia malengo yake na kubwa ambalo wanalihitaji ni kuondolewa kwa ukiritimba ambao upo kwenye baadhi ya taasisi za umma kiasi cha kukwamisha jitihada za kwanda hicho.Ameongeza tatizo si soko kwani lipo la uhakika kutokana na mahitaji ila tatizo ni ukiritimba lakini anaamini Serikali ya Rais Magufuli itatafuta ufumbuzi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad