HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 2, 2017

YANGA YAWAFUATA SINGIDA, NI VITA YA LWANDAMINA NA PLUIJM



KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Singida United Jumamosi Uwanja wa Namfua.



Yanga imeondoka bila kuwa na Lwachezaji wake wanne tegemeo ambao ni beki Juma Abdul, kiungo Thabani Kamusoko, washambuliaji Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe.

Kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia George Lwandamina kitavaana na Singida wanaonolewa na aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm.

Yanga inakwenda kwenye mchezo huo, ikitoka kutoa sare na wapinzani wa jadi, Simba kwa kufungana 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Uhuru.Sare hiyo imefanya timu hizo ziendelee kufungana kwa pointi 16 kileleni mwa Ligi Kuu, 16 kila moja sawa na Azam FC na Mtibwa Sugar. 

Mbali na Juma Abdul anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Ngoma, Tambwe na Kamosoku wao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi.
  

Ligi Kuu itaendelea Ijumaa, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Jumamosi Singida watakuwa wenyeji wa Yanga Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.


Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Jumapili kutakuwa na mechi mbili, mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad